KAMATI KUU YA CCM TAIFA YAMTEUA MOHAMED RAZA KUWA MGOMBEA WA NAFASI YA UWAKILISHI JIMBO LA UZINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMATI KUU YA CCM TAIFA YAMTEUA MOHAMED RAZA KUWA MGOMBEA WA NAFASI YA UWAKILISHI JIMBO LA UZINI

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kulia), akiendesha Kikako cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichokaa leo mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kuchagua mgombea atakayekiwakilisha Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mdogo wa Uwakilishi katika Jimbo la Uzini, ambapo Kamati hiyo imemtangaza Mohamed Raza kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM.
Kulia kwa Rais ni Makamu Mwenyekiti, Aman Abeid Karume, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed  Shein,  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Mjini Zanzibar leo Januari 12, 2012, wakati akitangaza rasmi matokeo ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa, kilichomteua, Mohamed Raza, kuwa mgombea wa nafasi ya Uwakilisho wa Jimbo la Uzini kupitia CCM.   
Nape alisema kuwa Kamati hiyo imeamua kumteua Raza kutokana na Kamati kujiridhisha kwa vigezo vyote husika ambapo alimtaja Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwa ndiye atakayezindua rasmi kampeni za uchaguzi huo unaotaraiwa kufanyika Februari 12 mwaka huu, ambapo pia kampeni hizo zitafungwa na Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa katika Kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages