Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akionesha Sheria
namba 4 ya mwaka 1976 ya Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza
kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa ufafanuzi wa
kuhusu sheria hyo kwa vyombo vya vya habari leo jijini Dares Salaam.
-----
Benjamin Sawe-Maelezo Dar es Salaam
Wasanii
wa Filamu na Michezo ya Kuigiza wameshauriwa kuzisoma nyaraka
mbalimbali za Bodi ya Filamu ili wajue sheria na kanuni zinazohusu
tasnia ya hiyo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini Joyce Fissoo alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya Sheria namba 4 ya
Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976.
Akifafanua
juu ya sheria hiyo, Bi Fissoo alisema ndiyo inayoendelea kutumika mpaka
sasa na kukanusha tuhuma zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari
kuwa ya uwepo wa matumizi ya sheria mpya.
“Hakuna
Sheria mpya ya Filamu na Michezo ya Kuigiza iliyotungwa, Sheria
inayoendelea kutumika ni ile ya mwaka 1976 bali kilichofanyika ni
utekelezaji wa kanuni za sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ambapo
mchakato wake ulianza mwaka 2011.
Akizungumzia juu ya malalamiko ya baadhi ya wasanii kushindwa kuhimili kulipa ada ya Sh. 500,000(laki tano) Bi. Fissoo
alisema kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinampa Waziri mwenye dhamana
husika kutoa msamaha wa malipo kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa
kiasi cha fedha hizo.
“Ada
wanayolipa wasanii ya Sh.500, 000 (laki tano) ipo toka siku za nyuma
ambapo Sheria namba 4 ya Filamu na Michezo ya kuigiza inampa mamlaka
Waziri husika kutoa msamaha kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa
ada hiyo”.alifafanua.
Alisema kwamba msamaha wa ada ya sh. 500,000 utatatolewa
pale tu msanii atakapotoa taarifa kwa Waziri husika na mara baada ya
kujiridhisha ndipo msamaha utatolewa na kutangazwa kwenye gazeti la
Serikali.
Amewashauri
wasanii wa Filamu kuwa Wazalendo kwa kutengeneza filamu zenye maadili
ya Mtanzania na si kutengeneza Filamu zenye maudhui ya kimagharibi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)