KAMANDA
WA POLISI MKOA WA ARUSHA BW THOBIAS ANDENGENYE AKIZIPANGA RISASI
AMBAZO ZILITUMIKA KATIKA TUKIO LA KUUA ASKARI KATIKA ENEO LA
SHANGARAI
Na Gladness Mushi
KATIKA hali isioyokuwa ya kawaida askari polisi F 228
Constebo Kijanda Mwandru amefariki dunia, pamoja na mkuu wa upelezi
wilaya Faustine Mwafele kujeruliwa vibaya na jambazi sugu mkoani hapa
ambaye amejulikana kwa jina la Hendry Samson Kaunda.
Akiongea
na waandishi wa habari mkoani hapa mapema leo kamanda wa polisi mkoa
wa arusha Andengenye Thobias alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo
majira ya saakumi za alfajiri.
Kamanda
Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo lilitokea mara baada ya
askari hao kwe nda kwa ajili ya upekuzi katika nyumba ya Bi Agness
Silas ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajili ya makazui ya majambazi
mjini hapa.
Alibainisha
kuwa mara baada ya askari hao kufika katika eneo la tukio kwa bahati
mbaya jambazi hendry aliwavamia askari hao na kisha kuwapiga kwa
risasi mfulululizo hali ambayo ilimsabbishia kifo askari huyo pamoja
na kumjerui Mrakibu huyo wa wilaya ya Arusha vijijini.
Pia alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi waliendelea na
msako mkali katika nyumba hiyo ya Bi Agness ambayo ilikuwa inasadikiwa
kuwaficha na kuwatunza majambazi na kisha kukuta vifaa mbalimbali
ambavyo vilikuwa vinatumika kwa ajili ya shuguli za ujambazi katika
maeneo mbalimbali hapa nchini.
Alitaja
Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na risasi 36,risasi 12 aina ya Short gun
,kitako kimoja cha bunduki aina ya Shortgun,pamoja na soksi za kuvaa
usoni ambazo walikuwa wakizitumia majambazi hayo katika shuguli
mbalimbali za uhalifu.
Bw Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto wawili
wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao
ni DainessMsawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye
aliyefumfungulia mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui askari polisi.
Aidha
mrakibu wa jeshi la polisi bado anaendelea na matibabu katika
hospitali ya Selian wakati polisi ikiendelea na msako dhidi ya
majmbazi hayo yaliyokimbia
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)