H-Baba katika pozi
MSANII
mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Ramadhan ‘H-Baba’
amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha,
akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza
Stone’ Mwalimu wa Walimu.
Akizungumza
na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni
miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya
itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia
sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha
alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika
Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya
kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba
alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu
tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti
murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja
studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni
pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar
es Salaam.
Pia
alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni
pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe
na Nimpende Nani.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)