Ndugu zangu,
Niliondoka
Singida Mjini saa kumi na moja alfajiri kuelekea Dodoma. Kilomita 40
kutoka Manyoni nilikutana na hali hiyo pichani kunako saa kumi na mbili
na nusu. Eneo la tukio niliwakuta askari watano wamevalia kiraia wakiwa
na silaha za moto. Wameniambia tukio limetokea usiku wa kuamkia leo
majira ya kuanzia saa sita usiku na linawahusisha maja majambazi
wasiopungua wanane.
Kuna
walioporwa fedha, simu na mali zao . Mahali hapa kuna pori kubwa upande
wa kushoto. Inaaminika majambazi hayo yenye silaha yangali yamejificha
porini.
Hakuna aliyekamatwa. Nilishuhudia polisi hao wakifuatilia nyayo huku wakinionyesha mahali majambazi hayo yalilala chini kujificha wakisubiri giza na kuanza kupanga mawe yao. Kwa kusoma mazingira ya eneo kwangu mimi napata tafsiri kuwa majambazi hayo yalifanya maandalizi ya mpango wao kwa siku kadhaa.
Maana,
mawe hayo mazito yanaonekana kuwa yalikuwa yakisogezwa usiku karibu na
tukio na kufikia idadi waliyohitaji. Intelijensia ya kipolisi ingefanya
kazi yake sawa sawa na kwa kushirikiana na wenyeji ingeweza kubaini
mapema movement ya mawe yale. Na katika dunia ya sasa , mbwa wa polisi
waliopewa mafunzo wangefanya kwa haraka na kwa ufanisi zoezi la
kufuatilia majambazi porini badala ya polisi kufuatilia nyayo kwa
macho.
Maggid Mjengwa,
Dodoma, Januari 27, 2012chanzo na http://www.mjengwablog.com/
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)