Wananchi wa Mombo na viongozi wa Serikali wakiangalia ajali hiyo
mbaya iliyotokea eneo la Nduu Mombo na kupoteza maisha kwa askari wawili
na kujeruhi askari wanne wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) Mkoa wa Tanga
wakati wakitokea Lushoto kwenye ziara ya makamu wa Rais Dkt. Mohamed
Bilal.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani Tanga wakipata
msaada wa kuvutwa kutoka kwenye bonde baada ya gari lao kuacha njia na
kuelekea bondeni wakati wakiwa kwenye msafara wa ziara ya makamu wa Rais Dkt.
Mohamed Balil eneo la Nduu Mombo lililopo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na
Korogwe jana na kusababisha vifo vya askari wawili wa kikosi
hiko cha kutuliza ghasia (FFU)
Mmoja wa Majeruhi wa ajali hiyo akiwa hospitalini tayari kwa kupata matibabu katika hospital ya Magunga wilayani Muheza
Viongozi wa Serikali na wananchi wa kijiji cha Nduu,Mombo mkoani
Tanga wakitafuta namna ya kuwatoa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia
(FFU) mkoani Tanga mara baada ya gari lao lenye namba za usajiri PT 2000
aina ya Toyota Land Crusser kuacha njia na kupindukia bondeni wakati
wakiwa kwenye ziara ya Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal ajali iliyotokea jana
eneo la Nduu Mombo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe.Picha Kwa Hisani Ya OTHMAN MICHUZI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)