EWURA Wapandisha Bei Ya Umeme Rasmi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

EWURA Wapandisha Bei Ya Umeme Rasmi

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Haruna Masebu
---
 
SIXTH FLOOR, HARBOURVIEW TOWERS, SAMORA AVENUE, P O BOX 72175 DAR ES SALAAM, TANZANIA
TEL: (+255-22) 2123850; 2123853; 2123854; 2123856; FAX:  (+255-22) 2123180
E-mail:  info@ewura.go.tz                 Website:  http.//www.ewura.go.tz
 

TAARIFA  KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU UAMUZI WA BODI YA EWURA JUU YA  MAOMBI YA DHARURA YA TANESCO YA KUPANDISHA BEI YA HUDUMA YA UMEME

Tarehe 9 Novemba 2011, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea maombi la dharura kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinishiwa ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 ya bei ya sasa. Maombi haya yalisajiliwa Namba TR-E-11­-012.
Kulingana na maombi yaliyowasilishwa,  katika mwaka 2010 na 2011 Tanzania ilikuwa na hali mbaya ya mvua katika maeneo ya mabwawa na hivyo iliathiri uzalishaji wa umeme. Hii ilisababisha nchi kuwa na upungufu mkubwa wa umeme na kuathiri sio tu hali ya kifedha ya TANESCO, bali pia na uchumi kwa ujumla wake.
Ili kumaliza tatizo hilo, TANESCO ilisaini mkataba  na IPTL kuzalisha Megawati 100 kwa kutumia mafuta mazito (HFO); ilisaini mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Symbion LLC kuzalisha Megawati 112 kutumia gesi asilia na mafuta; na ilisaini mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Aggreko kuzalisha Megawati 100 kutumia mafuta ya dizeli.
Vilevile, TANESCO inatekeleza mradi wake wa Megawati 150 ambao utatumia gesi asilia pamoja na mafuta (dual fuel plant) na mradi mwingine wa Megawati 70 ambao utatumia mafuta mazito (HFO).  Ukiacha miradi ya TANESCO ambayo itakamilika mwaka 2012, umeme unaozalishwa kupitia mikataba tajwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la mgao wa umeme hapa nchini. Hata hivyo, juhudi za kumaliza mgao wa umeme zimeongeza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji za TANESCO.
Katika kukabiliana na hali hiyo, TANESCO iliwasilisha maombi ya dharura EWURA ikiomba kuongeza bei za huduma zake kwa 155.
Kulingana na kifungu Na. 15(1)(3) cha Mwongozo wa Uwasilishaji Maombi ya Bei wa  mwaka 2009 (Tariff Application Guidelines of 2009), Waziri mwenye dhamana (kwa hali hii) wa Nishati na Madini, aliwasilisha Hati ya Dharura (Certificate of Urgency) EWURA ili maombi husika yaidhinishwe haraka na sio kwa utaratibu wa kawaida.
Tarehe 11 Novemba EWURA ilipokea Hati ya Dharura kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini na hivyo kuanza mchakato wa kupitia maombi ya TANESCO baada ya kupata maoni ya wadau.
Kulingana na Kifungu Na.19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 2 Desemba 2011,  EWURA ilifanya mkutano jijini Dar es Salaam wa kukusanya maoni ya wadau, kuweka maombi husika katika tovuti ya EWURA, pamoja na kuwaandikia wadau wachache ili waweze kutoa maoni yao kuhusu uhalali wa maombi yaliyowasilishwa na TANESCO. Pia maombi tajwa yalitangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali.
Baada ya kufanya uchambuzi wa maombi  yaliyowasilishwa pamoja na kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA ilikutana tarehe 12 Januari 2012 na kufanya uamuzi, pamoja na mambo mengine:
(a)  Serikali imechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kupunguza makali ya maisha kwa wa Tanzania kwa mosi; kufuta kodi ya mafuta kwenye mitambo, itakuwa inalipia Sh. bilioni 18  gharama za mitambo IPTL (Capacity Charges) na kusamehe deni la Sh. bilioni 136 kwa TANESCO.
(b) Kutokana na ukokotoaji uliofanywa na EWURA, kwa kuzingatia mzigo ambao Serikali imeubeba na pia kwa kuzingatia hali ya hewa ambayo inaweza kufanikisha upatikanaji wa mvua kwa wingi na hivyo kujaza kwenye mabwawa, bei ya umeme itaongezeka kwa wastani wa asilimia 40.29 kwa wateja wote isipokuwa wateja wanaotumia uniti 0 – 50 (0 – 50 kWh) kwa mwezi na ZECO, bei imepunguzwa kwa kwa asilimia 10.  Na wafanyakazi wa TANESCO watalipa kama wateja wengine.  Bei hizo  zitaongezeka kama inavyoonekana katika Jedwali hapa chini.
(c)  Bei zilizoidhinishwa zitaanza kutumika tarehe 15 January 2012 mpaka hapo uchambuzi wa kina utakapokamilika na hivyo kutolewa kwa Order nyingine.
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages