Na Mwandishi Wetu
MBUNIFU
anayekuja juu kwa kasi nchini, Doreen Estazia Noni amesema kuwa
atatumia aliyojifunza katika mkutano wa Uchumi Duniani kuendeleza fani
yake ya ubinifu wa mavazi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Noni
ambaye anamiliki lebo yake ya Eskado Bird alisema kuwa mkutano huo
umemfungua sana katika suala la kimaendeleo na kukuza kipato kutokana na
mafundisho yake.
Alisema
kuwa katika mkutano huo alishiriki kama mjasiliamali kupitia masuala ya
mavazi, aliweza kubadilishana mawazo na kuapata uzoefu mkubwa kutoka
kwa wachumi, wafanyabiashara maarufu duniani mbali ya wakuu wa nchi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa miongoni na tajiri maarufu duniani, Bill
Gates walikuwa miongoni mwa washiriki katika mkutano huo uliofanyika
nchini Uswis kuanzia Januari 25 mpaka 29.
“Najiona
kama nimezaliwa upya kutokana na yale niliyojifunza na kupata uzoefu
katika mkutano mkubwa wa Uchumi Duniani, nilikuwa miongoni mwa washiriki
vijana 70 kutoka nchi mbali mbali 36 duniani, najisikia faraja kuwa
kijana na mbunifu pekee wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika mkutano
huo,” alisema Noni.
Alisema
kuwa akiwa kama “Global Shapers”, aliweza kutoa mada mbalimbali ikiwa
pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa shule ijulikanyo kwa jina la Swiss
Alpine katika kipengele cha ujasiliamali.
Alifafanua
kuwa aliweza kubadilishana mawazo na wanafunzi hao kuhusiana na nini
anachokifanya ikiwa pamoja kuzungumzia lebo yake ya upande wa mavazi ya
Eskado Bird hasa kampeni ya mtindo wake ujulikanao kwa jina la What's
Your Freedom? (WYF?) .
Pia aliweza kuitambulisha kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Miracle Films and Studios Limited.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)