Mhe
Hamad Rashid,Mbunge wa Jimbo la Wawi akizungumza na Waandishi wa Habari
nje ya Ukumbi wa Mkutano muda mfupi baada ya kufukuzwa Uanachama wa
CUF,na Mkutano wa Baraza Kuu la CUF, unaofanyika katika Hoteli ya
Mazsons Shangani Unguja jana.
Naibu
Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara Julius Mtatiro,akitowa taarifa ya
Kikao cha Baraza Kuu hatuwa zilizochukuliwa kuwafukuza unanachama
wanachama wake wanne, Hamadi Rashid, Juma Said Sanani, Doyo Hassan
Doyo,Shoka Khamis na Yasin Mrotwa kupewa karipio kali.
Mwenyekiti
wa Serekali za Mitaa Mkunduge Tandale Dar-es-Salaam Tamim Omar Tamim,
akizungumza na Waandishi wa habari, wakati akisubiri kuitwa katika
Baraza Kuu kujieleza.
Mjumbe
wa Baraza Kuu la CUF, Shoka Khamis Juma, ambaye ni mmoja wa
Mwanachama aliyefukuzwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la CUF, akizungumza
na waandishi baada ya kutoka katika kikao kumaliza kujieleza.
Waandishi
wa habari wakiwa katika viwanja vya Hoteli ya Mazsons Shangali
wakisubiri yaliojiri ndani ya Kikao cha Baraza Kuu.Picha Zote na Othman
Mapara
--
BARAZA Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) limemvua uanachama Mbunge wa Wawi na Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, Hamad Rashid Mohamed, kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama na hivyo kupoteza sifa za uanachama.
Akitangaza uamuzi huo katika Hoteli ya Manson Mji Mkongwe jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro alisema mbali na Hamad Rashid, pia baraza hilo limewavua uanachama wajumbe wengine watatu wa Baraza Kuu.
Wajumbe hao ni Doyo Hassan Doyo kutoka katika Mkoa wa Tanga, Juma Sanani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na Shoka Khamis Juma, aliyewahi kuwa Mbunge wa Micheweni kwa tiketi ya CUF.
“Baraza Kuu la CUF limewafukuza viongozi hao baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili kutoka wajumbe wa Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka wajumbe Zanzibar,” alisema
Mtatiro.
Mjumbe mwingine: Yasin Mrotwa amepewa onyo kali na karipio huku na kwa mujibu wa Mtatiro, anaendelea kuchunguzwa na Baraza Kuu.
Seif dikteta!
Baada ya kuvuliwa uanachama, Hamad Rashid alizungumza na waandishi wa habari na kumuita Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, dikteta na kiongozi asiyeheshimu uamuzi wa Mahakama.
“Sisi tumeweka pingamizi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa mkutano wa Baraza Kuu na hati ya Mahakama ipo wanayo...sasa nawashangaa wanakiuka sijui kwa nini?” Alihoji Hamad Rashid.
Alisema watakwenda tena mahakamani Februari 14 kusikiliza shauri lao la pingamizi la kikao hicho.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)