Taswira Mbalimbaliza Maandamano ya Chadema Nchini
--
Ndugu wananchi na wakazi wa Arusha.
Tarehe 5 Januari ni siku ya kumbukumbu ya maana sana katika chama chetu kwenye mkoa wetu na halmashauri ya jiji letu la Arusha.
Tarehe
5 Januari mwaka 2011 ulifanyika mkutano mkubwa ambao ulikuwa umebeba
ujumbe wenye madai ya wananchi kuhusu ukiukwaji wa demokrasia katika
suala la uchaguzi wa UMEYA katika jiji la Arusha. Wakazi wa Arusha
walijitokeza kwa wingi kwa sababu walikuwa wameelewa nini hasa kilikuwa
kinalalamikiwa.
Kwa
yote yaliyotokea mwaka mmoja umepita sasa, chama kinawapa pole
makamanda wote na kuwataka tujipe moyo kwa safari ya ukombozi
tuliyoianza. Sote tufahamu kuwa iko siku tena sio muda mrefu wakazi wa
Arusha na Watanzania kwa ujumla tutafaidi matunda ya rasilimali zetu
nyingi ambazo kwa ujumla wake iwapo zitasimamiwa vizuri kwa haki na
usawa hatupaswi kuitwa maskini.
Tarehe
5 Januari, CHADEMA tulipaza sauti zetu tukiwa na madai ya msingi sana
ambayo yanabeba maisha ya wakazi wa Arusha. Suala la uchaguzi wa MEYA wa
jiji la Arusha ambao ulichakachuliwa kwa uwazi, makusudi na aibu kwa
waliotenda. Bado madai ya wakazi wa Arusha na chama kwa ujumla yanabaki
pale pale kuwa hatumtambui MEYA wa CCM aliyechaguliwa kwa mazingira
yasiyo ya haki.
Kwa
vile suala la maandamano lipo mahakamani, hatutalizungumzia, tunasubiri
haki na sheria vichukue mkondo wake katika kuamua kuhusu suala hilo.
Sambamba
na hili, tunawapongeza wakazi wa Arusha kwa ujasiri na umahiri wao
katika kupigania na kusimamia bila woga masuala ya msingi. Ujasiri huu
ndio unaopelekea wakazi wa Arusha kutokubali kunyanyaswa hasa inapokuja
kwenye masuala muhimu ya haki za binadamu.
Kwa
wakati wote hali ya Arusha katika uhalisi imeendelea kuwa ya amani na
utulivu na watu wamekuwa wakifanya shughuli zao kama kawaida licha
makada wa chama tawala CCM na baadhi ya viongozi wa serikali kutoa
maneno yenye utata kwa kuizungumzia hali ya kisiasa kwa sura ya kukejeli
demokrasia na haki za watu.
Tunaendelea
kuwasihi wakazi wa Arusha waendelee kuwa majasiri, waendelee kuwa
wachapakazi na kuwa tufanye kazi kwa kujituma kwa maendeleo yetu na ya
watoto wetu.
Mwaka
wa 2012 uwe ni mwaka wa kitofauti katika kuifanya Arusha yetu kwa
kuleta na kufikia mabadiliko chanya ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na
zaidi sana kushughulikia kwa dhati suala la ajira kwa wasio na ajira.
Amani Golugwa
KATIBU WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)