Kaimu
Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Lebejo akisisitiza jambo kwenye
programu ya Jukwaa la Sanaa inayofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza
hilo Ilala Sharif Shamba na kuhudhuriwa na wadau wa Sanaa. Kulia kwake
ni Afisa Uhusiano wa Uhamiaji Bi. Tatu Burhan.
Ssp
Edson Kasekwa kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu, Kitengo maalum cha
Operesheni uzuiaji uhalifu akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu
matumizi ya Sanaa katika Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi. Kulia kwake
ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa, BASATA Bi. Vivian Shalua.
Afisa
Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan akieleza haja ya Jamii
kushirkiana na Idara yake katika kupambana na tatizo la Uhamiaji haramu
nchini. Kushoto kwake ni Bw. Lebejo.
Kikundi
cha Ngoma cha Jeshi la Polisi kikitumbuiza kwenye Programu ya Jukwaa la
Sanaa ambapo elimu kuhusu dhana ya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii
ilitolewa kwa Wadau zaidi ya 140.
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi la Polisi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Programu hiyo ya Jukwaa la Sanaa.
Mkongwe
wa Sanaa za Maonyesho Mzee Nkwama Bhallanga akielezea masuala
mbalimbali kuhusu Sanaa Shirikishi katika Polisi Jamii na Ulinzi
Shirikishi.
Wadau wa Sanaa wakiifuatilia Programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii.
======= ====== =======
BASATA, JESHI LA POLISI WAUNDA KIKOSIKAZI KUDHIBITI UHARAMIA KWENYE SANAA
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) na Jeshi la Polisi nchini wameunda
kikosikazi maalum kitakachokuwa kikifuatilia uharamia na maovu
mbalimbali katika shughuli za Sanaa na Burudani.
Kikosikazi
hicho kimeundwa baada ya Jeshi la Polisi nchini kutumia Sanaa
shirikishi katika kutoa elimu kwa wadau wa Sanaa kuhusu dhana ya polisi
jamii na ulinzi shirikishi kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila
wiki makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.
Akizungumza
kuhusu kikosikazi hicho, Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa, BASATA Bi. Vivian
Shalua alisema kuwa, kazi kubwa ya kikosi hiki itakuwa ni kufuatilia
maonesho yasiyokuwa na vibali, uharamia kwenye kazi za wasanii na
wasanii kutoka nje wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
Aliyataja
majukumu mengine ya kikosikazi hicho kuwa ni pamoja na kudhibiti
maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania, kusimamia utoaji
vibali kwa wasanii wa kitanzania wanaoenda kufanya maonesho nje ya nchi
na majukumu mengine yatakayojitokeza.
“Kikosikazi
hiki kitakuwa tayari kufuatilia taarifa yoyote ya uharamia kwenye kazi
za wasanii, maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania na
wasanii wanaoingia ndani ya nchi na kufanya maonesho bila vibali”
alisisitiza Shalua.
Kikosikazi
hicho kinaundwa na Shani Kitogo (Afisa Utamaduni Ilala), Tatia Ramadhan
(Polisi, TAZARA), Afande Jeremiah (Polisi Kati), Koplo Juma Mashauri
(Polisi Airport), Michael Kagondela (Idara ya Utamaduni), Afande Deus
Matoro (Reli) na Afande Swai (Traffic),
Wengine
ni Vivian Shalua (BASATA), Jonathan Abel na Tatu Burhan (Uhamiaji),
Deus Kessy (Polisi Reli), Koplo Josephat Syllively (Polisi – Maji),
Masanja Nyalali (Polisi – Airport) na PC Mwakajaby (Polisi – TAZARA)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)