Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionyesha baadhi ya ramani yenye michoro
ya barabara za juu (Flying- Over) zitakazojengwa jijini Dar es Salaam.
mbele ya waandishi wa habari na Wadau wa sekta ua Ujenzi leo,wakati ya
hafla ya uwekaji wa sahihi ya Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mfumo wa
Usafiri haraka wa mabasi jijini Dar es salaam.awamu ya kwanza,Kandarasi
ya kwanza (barabara),utakapo kamilika ujenzi wa barabara hizo itasaidia
kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salam,ambapo ndio lengo
kubwa la serikali.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale
(kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG
INTERNATIONAL Gmb ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia)
wakibadilishana hati za mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa
Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi
wa Kwanza (Barabara) Nov.22.2011 katika makao Makuu ya Wizara ya
Ujenzi,.Mradi huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia
ambapo mradi mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa
awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9
katika barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara
ya Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi
(kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa
na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya
Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi,
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale
(kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG
INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia) wakitiliana
saini mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa
Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza
(Barabara) Nov.22.2011 katika makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi,. Mradi
huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi
mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa awamu ya
kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9 katika
barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara ya
Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka
Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya
Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi.
Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO
Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)