Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.
--
Kuchangia 30Mil. Wateja wake kuchangia kupitia Red Alert na m-pesa.
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepokea kwa masikito makubwa
taarifa za mafuriko na kusababisha maafa yaliyoukumba mkoa wa Dar es
salaam na kugharimu maisha ya watu kufutia mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha mkoani humo na sehemu nyengine za nchi.
Hali
hii inatoa uhitaji wa taifa kushikamana na kukaa pamoja katika
kuwafariji wafiwa na wale ambao walioguswa na athari za maafa hayo kwa
namna moja ama nyingine.
“Tunafuatilia
kwa karibu taarifa za maafa haya. Tumeguswa na vifo vya watanzania
wenzetu waliopoteza maisha na tunatoa pole kwa wafiwa na tunawafariji
wote waliothiriwa na maafa haya”Alisema Ofisa Mkuu wa Masoko na
Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.
Vodacom
tayari imeshachukua hatua za awali za dharura kusaidia waathirika na
itatumia shilingi Milioni 30 kutoka mfuko wake wa kusaidia jamii wa
Vodacom Foundation.
“Kwa
sasa tunafanya mawasiliano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambae ndie
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa kupata mahitaji muhimu ya haraka ili
tuweze kutumia fedha hizo. Tunatarajia kukamilisha mchakato huu kwa
haraka iwezekanavyo kutoa unafuu wa maisha kwa waathirika.”Amebainisha
Mwamvita
Aidha
kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake kuungana na
Menejimenti na wafanyakazi wake kuonesha kuguswa kwao kwa kuchangia
walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa
njia ya m-pesa.
Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.
“Tunaimani
kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa
kitaifa unaojenga tunu ya utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa
wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina”.
Amesema Mwamvita.
Michango
yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya
Maafa ya mkoa kuongeza Nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na
kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.
Aidha
kampuni ya Vodacom Tanzania inavipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na
usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi
hatua ambayo bila shaka imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)