Waraka wa Pili wa Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo la Ubungo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waraka wa Pili wa Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo la Ubungo

Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh John Mnyika

Uhuru na Kazi:
Nimekuja kuwatembelea kuona hali halisi ya uharibifu wa makazi yenu, mali zenu na miundombinu yetu kutokana na maafa ya maafuriko katika mitaa hii ya kata ya mabibo. Kuanzia maafa yatokee tarehe 20 Disemba mpaka tarehe 24 Disemba nimekuwa pamoja na wananchi wenzangu wa jimbo la Ubungo bega kwa bega katika jitihada za uokoaji na utoaji wa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali mathalani Msewe, Ubungo, Kisiwani, Kibo, Mburahati, Sinza D, Sinza E, Uzuri, Manzese Chakula Bora, Mburahati Kisiwani, Msigani, Mbezi Kibanda cha Mkaa, Kimara B. Na pia, nimeenda kutoa misaada kwa majimbo jirani ya Kinondoni (Magomeni Sunna na Kigogo), Kawe (Msasani Bonde la Mpunga na Bunju) na Ilala (Mchikichini). Kutokufika Mabibo, katika hizo siku chache, kunadhihirisha ukubwa wa maafa yenyewe na ilikuwa vigumu kuwepo mahali pote wakati wote. Hata hivyo, katika wakati huo wote nilikuwa na mawasiliano na wananchi na viongozi kuhakikisha kwamba mamlaka zinazohusika na uokoaji zinafika katika maeneo haya. Nawashukuru wote mliotoa ushirikiano wakati wa uokoaji na nawashukuru pia mliotoa msaada wa hali na mali kwa majirani zenu katika kipindi hiki kigumu.

Nimekuja kwenu leo katika sikukuu ya kufungua zawadi (boxing day) kutoa michango yangu ya chakula na mavazi kwa waathirika wa maafa wasio na uwezo; hata hivyo zawadi yangu kubwa kwenu leo; sio vitu hivi tulivyotoa, ni waraka ninaoutoa kwenu wananchi wenzangu wa jimbo la Ubungo. Waraka huu naamini utakuwa ‘chakula’ cha fikra kwenu leo na kesho kwa ajili ya mabadiliko katika maisha yetu na taifa letu.

Katika waraka wangu wa kwanza kwenu niliwapa mrejesho kuhusu uwakilishi wa Mbunge katika mkutano wa pili wa Bunge. Nawaandikia waraka huu “Uhuru na Mabadiliko” katika mwaka 2011 wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa inaitwa Tanzania bara.

Lengo la waraka huu ni kuungana nanyi katika mwaka huu kutafakari kila mmoja wetu kuhusu taifa letu lilipotoka, lilipo na tunapotaka liende katika kipindi cha miaka 50 toka Uhuru na kutumia fursa hiyo pia kutafakari kuhusu jimbo letu katika kipindi cha mwaka mmoja toka uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2012.

Waraka huu wote, isipokuwa aya ya kwanza na aya hii ya tatu, niliuandika tarehe 9 Disemba 2011; hata hivyo sikuutoa siku hiyo kutokana na ‘macho na masikio’ ya wengi kuelekezwa katika ‘sherehe’ za siku hiyo pamoja na matarajio kuhusu hotuba ya Mkuu wa Nchi kugusa masuala mapana kuhusu mwelekeo wa taifa. Nimeona niutoe waraka huu katika kipindi cha kuelekea mwisho wa mwaka, na ni wakati muafaka wa kutafakari zaidi baada ya ‘sherehe’ kwa kuwa mpaka sasa Rais Jakaya Kikwete hajatoa hotuba nyingine ndefu kama alivyoahidi tarehe 9 Disemba na pia taifa linamaliza majonzi yaliyotokana na maafuriko yaliyoleta maafa katika mkoa wa Dar es salaam
Kwa kuendelea Kuisoma <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages