Meneja
Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (kushoto) na
Ofisa wa Mfuko wa Kusaidia Jamii wa kampuni hiyo, Grace Lyon, wakishusha
viloba vya mchele, unga wa sembe,sukari na maharage vilivyotolewa na
Vodacom kusaidia kambi ya waathirika wa mafuriko ya Dar es salaam ya
Hananasifu juzi. Wa kwanza kulia ni Mfanyakazi wa Vodacom, Lilian Kisamba, akisadiana na wasimamizi wa kambi hiyo kupokea vyakula hivyo.
Mkuu
wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, (kulia) akimtiwsha Mjumbe
wa Serikali ya Mtaa wa Mkunguni B, kata ya Hananasifu, Andrew Mkude
kiloba cha sukari. Vodacom ilikabidhi mchele, sukari, unga wa sembe,
mikate na maji ya kunywa kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam
wanaojihifadhi katika kambi ya Hananasifu juzi.
Ofisa
wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, akisaidiana na mmoja wa wasimamizi
wa kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam kambi ya Green Acre
Magomeni kubeba kiloba cha mchele tayari kukabidhiwa kwa waathirika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)