Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Jordan Rugimbana akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa duka jipya la kisasa la kampuni ya Vodacom lilipo
katika jengo la Quality Center barabara ya Pugu jijini Dar es salaam
litakalotoa huduma kwa wateja pamoja na mauzo ya bidhaa mbalimbali za
Vodacom. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Pwani Bw. Henry
Tzamburakis.Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa huduma za mauzo ya rejareja wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bi.
Upendo Richard akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Jordan
Rugimbana bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika duka jipya la mauzo na
huduma kwa wateja la kampuni ya Vodacom mara baada ya kulizindua rasmi
mwishoni mwa wiki. Duka hilo la kisasa lipo katika jengo la Quality
Center, barabara ya Pugu na litatoa huduma za aina zote kwa wateja wa
Vodacom.
Mkuu
wa Wilaya Kinondoni Jordan Rugimbana akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu
wa huduma za mauzo ya rejareja wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bi.
Upendo Richard jinsi ya kutumia Web Box kifaa maalum kinachowezesha
matumizi ya kompyuta kupitia televisheni muda mfupi baada ya Mkuu wa
Wilaya kuzindua duka jipya la kisasa la Vodacom lililopo katika jengo
la Quality Center, barabara ya Pugu jijini Dar es salaam mwishoni mwaka
wiki.Kulia ni Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Pwani Bw. Henry
Tzamburakis.
--
Kampuni
ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua duka jipya la kisasa
lililopo katika jengo la kibiashara la Quality Center, kwa ajili ya
kuhudumia wateja wake pamoja na kufanya mauzo likilenga kusogeza karibu
zaidi huduma kwa wateja wake.
Akizindua
duka hilo mwishoni mwa wiki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan
Rugimbana alisifu juhudi za Vodacom za kutoa huduma bora kwa wateja huku
akiwataka kuongeza ubunifu ili kuwanufaisha watumiaji wa huduma za
simu za mkononi nchini.
“Nimefurahi
kuwa hapa leo kuzindua duka lenu, nawapongeza kwa juhudi zenu za dhati
mnazozifanya katika kutoa huduma bora na namna mnavyowahudumia wateja
wenu na uwepo wa duka hili utapanua wigo wa kuwahudumia kwa uharaka,
urahisi na ukaribu zaidi”Alisema Rugimbana muda mfupi baada ya kufanya
uzinduo huo na kupata fursa ya kutembelea duka hilo lililopo barabara ya
pugu jijini Dar es salaam.
Mkuu
huyo wa Wilaya amesema mpangilio wa duka hilo pamoja na mahali lilipo
ni wazi litatoa faida kubwa kwa jamii na wateja wa Vodacom kampuni
inayoongoza soko la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi kwa kuwa na
wateja zaidi ya milioni kumi na moja.
“Kadri
mnavyosogeza huduma zenu karibu na wateja ndivyo hivyo mnavyoongeza
urahisi wa maisha kwa wateja ambao bila ya hivyo watalazimika kusafiri
umbali mrefu kufuata maduka hayo ili waweze kupata huduma ikiwemo
kutatuliwa matatizo wanayokabiliana nayo katika kutumia huduma za
mawasiliano ya simu”Aliongeza Rugimbana huku akitoa rai kwa wananchi
kutumia fursa za maduka hayo kuwa karibu nao kujipatia huduma na
kujifunza.
Awali
akimpatia maelezo Mkuu wa Wilaya. Meneja Mauzo wa kampuni ya Vodacom
Kanda ya Pwani Bw. Henry Tzamburakis alisema kufunguliwa kwa duka hilo
kunalenga kutoa urahisi kwa wateja wa Vodacom kupata huduma bora.
Amesema
hilo ni duka la kumi na moja katika mkoa wa Dar es salaam mbali na
maduka madogo madogo yaliyozagaa kila kona yanaitwa Vodacom Duka ambayo
kwa pamoja yanatenegza mtandao mpana wa kuhudumia wateja na jamii kwa
ujumla kwa ukaribu zaidi katika kiwango cha ubora wa hali ya juu
“Hili
ni duka letu la kumi na moja katika mkoa wa Dar es salaam ni azma ya
Vodacom kuona kwamba mteja anahudumiwa na kufikiwa na huduma kwa uharaka
na urahisi zaidi ili waweze kujiskia ufaghari kuwa miongoni mwa
familia kubwa ya wateja zaidi ya milioni kumi na moja”Alisema
Tzamburakis.
Amesema
ukuaji wa Vodacom katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi
unachagizwa pamoja na mambo mengine na udhati wa kampuni hiyo katika
kuwahudumia wateja wake kwa kiwango cha ubora unaoendana na hadhi ya
kampuni bila kujali aina ya mteja anaehudumiwa kwa kuzingatia kwamba
kila mteja wa Vodacom ana haki sawa ya kupata huduma bora zitakomfanya
mwisho wa siku kutabasamu.
“Tumethubutu
kuleta duka hili katika eneo hili la biashara tukiamini litawahudumia
vema wateja wetu wa maaeneo ya Buguruni,Gongolamboto, Chang’ombe, na
maeneo mengine ya Wilaya ya Temeka na Ilala hivyo ni imani yetu kwamba
kwa hatua hii wataendelea kujivunia kuwa wateja wa kampuni ya
Vodacom”Alisema Tzamburakis
Tzamburakis
amesema Amesema duka hilo litatoa huduama zote kwa wateja ikiwemo
huduima za M-PESA, usajili, manunuzi ya muda wa hewani na bidhaa
mbalimbali za Vodacom ikiwemo WEB BOX simu za mkononi na Moderm na
kwamba ni azma ya Vodacom kuimarisha mtandao wa maduka yake nchi nzima
ili kuendana na kasi ya ukuaji kibiashara na mahitaji ya wateja sokoni.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)