Mkuu
wa wilaya ya Mbeya Evans Balama akikabidhi vifaa vya shule kwa watoto
yatima na wenye uhitaji maalum wa mkoani Mbeya vilivyotolewa na kampuni
ya simu ya Vodacom kupitia kampeni yake ya Share&Care. Jumla ya
watoto mia tano walinufaika na msaada huo ambapo pia vituo kumi na
vitano vya kuelela watoto hao vilipatiwa vyakula katika hafla
iliyoambatana na chakula cha mchana. Kulia ni Mkuu wa mfuko wa jamii wa
Vodacom Yessaya Mwakifulefule na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa
Vodacom Kanda ya Kusini Bw. Jackson Kiswaga
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakionesha upendo kwa
watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu pamoja na baadhi ya
wazazi na walezi wa vituo vya yatima vya mjini Mbeya kwa kuwahudumia.
Vodacom kanda ya kusini mwishoni mwa wiki iliandaa tafrija kubwa ya
chakula cha mchana kwa watoto yatima zaidi ya mia tano ambao pia
walipatiwa zawadi za vyakula kwa ajili ya vituo vinavyowalea, sare za
shule na vifaa mbalimbali vya shule kupitia kampeni ya Vodacom
Share& Care.
Wafanyakazi
wa kampuni ya Vodacom mkoani Mbeya wakijumuika pamoja na watoto yatima
na waishio katika mazingira magumu kucheza muziki mara baada ya kupata
chakula cha mchana na watoto hao pia kukabidhi zawadi za vyakula na
vifaa vya shule kwa ajili ya ya krismasi kwa watoto hao zaidi ya mia
tano mwishoni mwa wiki. hafla hiyo ni mwendelezo wa kampeni ya Vodacom
Share & Care ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni hamsini
kwa mikoa mitano.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)