Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed
Shein akikabidhi kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwa wachezaji
wa timu ya Uganda (The Cranes) mara baada ya timu hiyo kushinda kombe
hilo kwa kuifunga timu ya Rwanda (Amavubi) katika mchezo uliofanyika
kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam.
Ilikuwa ni fainali ya kuvutia kwa timu zote mbili kutokana na kiwango
kilichoonyeshwa katika dakika 90, timu hizo zilitoka suluhu ya magoli
2-2 ambapo dakika 30 ziliongezwa lakini hazikuzaa matunda kwa timu zote
mbili, mpaka ilipofika wakati wa mikwaju ya penati, timu ya Uganda
ilipata penati 4-3 dhidi ya Rwanda, hivyo Uganda kutawazwa mabingwa
wapya wa kombe hilo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed
Shein akimpongeza mmoja wa wachezaji wa timu ya Uganda baada ya timu
hiyo kuwa mabingwa wapya wa TUSKER CHALLENGE CUP 2011.
Wachezaji wa Rwanda wakiwa haamini kilichotokea mara baada ya mpira kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Kutoka kulia ni Carol, Moureen na Bahati kutoka R&R wakiwa na baadhi ya warembo wakifurahi baada ya kumaliza kazi.
Wadau kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti na R&R wakifurahia kumalizika kwa kazi ya mashindano hayo kwa mafanikio.
Katikati
ni Richard Wells Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti akiwa
katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim
Mafuru na Moses Kebba Meneja Masoko wa Tusker Lager.
Zawadi
zikiandaliwa kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni
ya bia ya Serengeti na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo
Ephraim Mafuru.
Wachezaji
wa Uganda kulia na Rwanda wakichuana vikali kuwania mpira wakati timu
hizo zilipokutana katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)