Naibu
Kamishna wa Kodi za Ndani, Christine Shekidele (kulia), akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kususiana na Ongezeko la Thamani (VAT)
na faida zake kwa Taifa
Mkurugenzi
wa Fedha TRA, Saleh B. Mashoro akitoa maelezo juu ya mpango wa
mamlaka hiyo wa kukusanya Ongezeko la Thamani kwa wageni
watakaosafirisha bidhaa za ndani kupeleka nje ya nchi
Na Emmanuel Kimweri wa Fullshangwe - Dar es salaam.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), kuanzia tarehe 1, Januari 2012 inaanza
rasmi kushughulikia marejesho ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wasafiri wakigeni wanaondoka kwenda nchi za nje kwa mujibu wa sheria ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha
TRA, Saleh B. Mashoro, alisema utaratibu huu wa kukusanya VAT umekuwa
ukitumika na nchi mbalimbali duniani kutokana na ukweli kuwa VAT ni
kodi inayotokana na matumizi.
“TRA
imevuka malengo ya mwaka kwa kukusanya shilingi trillion mbili,
bilioni nne na sabini na na tano (Trilioni 2.475 bilioni) malengo ni
kukusanya trilioni mbili, bilioni nne na sabini na nne (Trilioni 2.474)
hii ni kuanzia Novemba mwaka jana hadi sasa”, alisema Mashoro.
Alisema
VAT itakayotozwa kwa wageni pindi watakapo safirisha bidhaa kutoa
ndani ya nchi kupeleka nje ya nchi kwa kuthibitishwa na maasira wa TRA
kuwa bidhaa hiyo haijatumika.
“Gharama ya marejesho ni asilimia tano (5%), ya kiasi cha marejesho na gharama hii italipwa na muombaji wa marejesho’ alisema
Aliendelea
kusema katika kuhakikisha zoezi lina kwenda vizuri tumeweka Wakala wa
Marejesho ambao ni Benki ya TWIGA BANCORP ambayo itakuwa na ofisi
zake katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (DIA) na Kilimanjaro
(KIA)
Aidha,
Mamlaka inawataka wale wote ambao wanaostahili kudai marejesho
sanjari na umma wote kwa ujumla wake kushirikiana na TRA ili kutoa
huduma bora yenye ufanisi wa hali ya juu kwa kuzingati sheria zinazohusika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)