Singida.
NAIBU
waziri wa maji, Mhandisi, Gerson Lwenge, ameitaka kampuni ya Spencon
Service Ltd ya Kenya, kukamilisha mradi wa maji hadi kufikia Juni
mwakani, ili wananchi wa mji huo waweze kunufaika nao.
Mradi
huo unagharimu jumla ya Sh.Bilioni 25.8, Mjini Singida,unasimamiwa na
mhandisi mshauri, kampuni ya M/s Don Consult Ltd, kwa ushirikiano na
Ewarema, zote za hapa nchini Tanzania.
Baada
ya kupata maelezo ya Mamlaka ya Maji safi na Maji taka(SUWASA) na
mhandisi mshauri (Don Cunsult), Naibu Waziri aliagiza mkandarasi huyo,
akamilishe kazi hiyo Juni, mwakani, ili serikali iendelee na mipango
mingine.
Mkurugenzi
wa SUWASA, Kombe Mushi, alisema Mradi huo, ulioanza Novemba 2009,
ulitakiwa kuwa tayari Novemba mwaka huu, lakini hadi sasa, upo nyuma
asilimia 60.
Mwaka
2003, zaidi ya Sh.Bilioni 15.7, zilitolewa mkopo na Benki ya
Kiarabu(BADEA) na Shirika la Mafuta Ulimwenguni(OFID),ili kutekeleza
mradi huo, lakini hadi sasa ni miaka minane tangu zitolewe, fedha hizo
hazijatumika ipasavyo, kutoka na sababu ambazo hazipo wazi.
Pia kiasi kingine cha zaidi ya Sh.Bilioni 10, kilitolewa na serikali ya
Tanzania kwa kushirikiana na programu ya maendeleo ya sekta ya Maji
nchini(WSDP) na kufanya jumla ya Sh.Bilioni 25.8, kwa ajili ya kuunga
mkono utekelezaji wa mpango, wa mradi huo. Na Elisante John
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)