TANZANIA FULL SCHOLARSHIP @ WESTMINSTER UNIVERSITY UK. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANZANIA FULL SCHOLARSHIP @ WESTMINSTER UNIVERSITY UK.

Ndugu zangu watanzania, chuo cha Westminster kilichopo katikati ya jiji la london, UK, kila mwaka kinatoa scholarship kwa watanzania kusoma degree ya kwanza na ya pili bure (unalipiwa ndege kwenda london na kurudi Tanzania, maradhi, chakula, ada yote na kila mwezi hela ya matumizi).

Tatizo hizi habari tukipata hatupeani, mwisho nafasi kama hizi zinafutwa chuoni maana hamna wanaoziomba.

Mi nilifanikiwa kuipata kupitia rafiki yangu, nami nimekuwa naitangaza na ntaendelea. Hii nafasi itasaidia kubadilisha maendeleo ya watanzania na Maisha yao kiujumla.

Link hiyo chini inamaelezo yoote. Deadline ni mwakani April, so kama upo interested, tumia mda huu kudownload form za kuomba chuo, ukipata chuo, then unaomba scholarship, maelezo yapo kwenye website yao www.westminster.ac.uk link ni http://2009.westminster.ac.uk/study/international/country-pages/africa/tanzania
Goodluck
Evelyn Kaijage

"Asante sana Evelyn kwa kutuhabarisha maana si wengi wenye moyo kama huu. Mungu akubariki."
TAFADHALI MJULISHE NA MWENZIO UONAPO HABARI HII!
Asanteni sana

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages