Mmoja wa wachezaji wa Stars, Nadir Haroub, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya moja ya mchezo wa timu hiyo hivi karibuni.
**************************************
Timu
ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeomba kucheza mechi
moja ya kirafiki na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Mechi hiyo
itafanyika Februari 23 mwakani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
DRC
inatarajia kuwasili nchini Februari 18 mwaka huu ambapo itaweka kambi
yake ya mazoezi hadi Februari 25 mwaka huu kujiandaa kwa mechi yao ya
mchujo ya Kombe la Afrika (CAN) dhidi ya Mauritius.
Mechi
ya DRC na Mauritius itachezwa Februari 29 mwakani nchini Mauritius.
Stars yenyewe itacheza mechi ya kwanza ya mchujo kwa ajili ya fainali
hizo za 2012 zitakazofanyika Afrika Kusini dhidi ya Msumbiji. Mechi hiyo
itachezwa Februari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WAKATI HUO HUO, 13 WASHIRIKI KOZI YA UKAMISHNA
Kozi
ya siku mbili ya ukamishna iliyomalizika Desemba 29 mwaka huu
imeshirikisha washiriki 13 chini ya ukufunzi wa Stanley Lugenge, Leslie
Liunda na Sunday Kayuni.
Walioshiriki
kozi hiyo ni Abdallah Zungo, Ally Mkomwa, Ally Mozi, Army Sentimea,
Awadi Nchimbi, Beatus Manga, Christopher Mpangala, Hakim Byemba,
Josephat Magazi, Juma Mgunda, Juma Mpuya, Mugisha Galibona, Ramadhan
Mahano, Robert Kalyahe na Said Nassoro.
Wakufunzi
wanaendelea kusahihisha mitihani ya washiriki na baada ya kazi hiyo kwa
ambao watakuwa wamefanya vizuri majina yao yataingizwa katika orodha ya
makamishna kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano
mengine yanayosimamiwa moja kwa moja na TFF.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)