Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea kwa
masikitiko taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mhariri Mtendaji
wa Kampuni ya Free Media Bw. Absalom Kibanda ya kujitoa kwenye Kamati
ya Taifa ya kukamilisha mchakato wa kupata vazi la Taifa, Wizara haina
pingamizi na uamuzi wake huo.
Wizara imesikitishwa na sehemu ya tamko lake kudai kuwa namnukuu,
“Nimelazimika kufikia uamuzi huu, baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na kufunguliwa mashitaka na Polisi na hatimaye kufikishwa kwangu Mahakamani usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri Nchimbi”, mwisho wa nukuu.
Kwa taarifa hii Wizara inapenda kuutarifu umma kuwa Habari hiyo ni uzushi usio na mashiko wenye nia ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Wizara na wadau wa Habari nchini.
Kwa mujibu wa majukumu ya Wizara, si sehemu ya kazi za wizara hii kushauri, kuchunguza au kuandaa tuhuma za makosa ya jinai. Ni vema iwe wazi kuwa Wizara hii, viongozi , watendaji, na watumishi wake hawajashiriki, hawajashirikishwa na hawajajishirikisha na hawajashauri wala kushauriwa juu ya tuhuma na mashitaka dhidi ya Bw. Kibanda.
Wizara inavisihi vyombo vya Habari kuendelea kuzingatia weledi, mila na desturi zetu katika kutekeleza majukumu yake.
Imetolewa na,
Msemaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Desemba 2011

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)