Rais
Jakaya Kikwete akiwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib
Bilal na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mara baada ya kurejea jijjini Dar
es salaam kutoka Kampala, Uganda, alikohudhuria mkutano wa siku mbili wa
wakuu wa nchi za maziwa makuu

Rais
Jakaya Kikwete akiagwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mh
Nsavike G. Ndatta katika uwanja wa ndege wa Entebbe leo Desemba 17,
2011 asubuhi wakati akiondoka Uganda kurejea nyumbani baada ya
kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu
Rais
Jakaya Kikwete akiwakabidhi Bw. Clement A. Chagula na bintiye Olivia A.
Chagula medali kwa niaba ya baba na babu yao Marehemu Dkt. Wilbert
Chagula, ambaye aikuwa ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya awamu ya
kwanza na mmoja wa watu maarufu waliotunukiwa nishani katika
kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Bw Chagula, ambaye ni mtoto wa marehemu,
hakuweza kufika Dar es salaam kupokea medali hiyo na Rais alipokuwa
Kampala akatumia nafasi hiyo kumpatia leo asubuhi katika hoteli ya Speke
Commonwealth Resort.







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)