Jaji Mstaafu Damian Lubuv |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Aidha,
Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid
kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius
Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Taarifa
iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi,
Bwana Phillemon Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo
umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.
Kabla
ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya
Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Baraza la Maadili ya Viongozi.
Mheshimiwa
Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis
Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai,
mwaka huu, 2011.
Naye
Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya
kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji
Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye
akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Naye
Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya
Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali. Bw. Mallaba anajaza nafasi
iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa
utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)