Marehemu Septi Suleiman amezikwa katika makaburi ya familia huko Mwera Kichokani leo.
Wananchi
mbalimbali wakiwa wamebeba mwili wa aliekuwakatibu mtendaji wa Tume ya
Utangazaji zanzibar na mwanahabari mkongwe Marehemu Septi Suleiman
ambaye amezikwa huko kijijini kwao Mwera Kichokani.
Wananchi
mabalimbali wakisali sala ya maiti ili kumuombea Marehemu Septi
Suleiman aliefariki leo katika Hospitali ya mnazi mmoja huko
Zanzibar.Picha Zote na Yusuph Simal,Maelezo-Zanzibar
----
Na Fatma Mzee Maelezo Zanzibar
Mamia
ya wananchi wa Zanzibar wa Kike na Kiume leo asubuhi walishiriki katika
mazishi ya mtangazaji mkongwe Septi Sulemein Juma aliezikwa kijijini
kwao Mwera nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mazishi
hayo yalihuzuriwa na watangazaji mbalimbali wa Zanzibar pamoja na
wakurungenzi wa vyombo mbali mbali vya habari vikiwemo vya utangazaji na
magezeti wakiongozwa na mkurugenzi wa habari maelezo Zanzibar Yussuf
Omar Chunda.
Marehemu
Septi alianza kazi ya utangazaji mnamo mwaka 1964 katika idara ya
habari na utangazaji katika semu ya Sauti ya Tanzania Zanzibar akiwa
mtangazaji mwanafunzi .Baadae alikwenda China katika idhaa ya Kiswahili
ya Redio China Kimataifa kwa muda wa miaka mitatu.
Alirejea
Zanzibar mnamo mwaka 1976 kuendelea na kazi katika Sauti ya Tanzania
Zanzibar .Septi Suleiman baadae aliwacha kazi ya utangazaji na kujiunga
na vyama vya wafanya kazi vya OTTU Tanzania.
Mnamo
mwaka 1996 aliteuliwa kuwa Mkurungenzi wa Idara ya Sauti ya Tanzania
Zanzibar katika mwenzi wa May ambapo kazi hiyo aliendelea nayo mpaka
mwaka 2001 ambapo aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji
Zanzibar.
Alistaafu
kazi katika mwaka 2006 ambapo baadae alifanya kazi akiwa Mkurugenzi wa
redio ya Adhana Zanzibar mpaka kifo kilipo mtokea.
Marehemu Septi Suleiman Juma amefariki akiwa na umri wa miaka 69 na ameacha mke na watoto 4 .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)