Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe
--
Leo(Jana)
kwa masikitiko makubwa sana nimesoma kwenye vyombo vya habari kwamba
ndugu David Kafulila kavuliwa uanachama wa chama chake. Kwa hatua hii
David anakuwa amepoteza Ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini licha ya kwamba
alichaguliwa na wananchi bila kujali vyama (NCCR-M wanachama wake huko
Kigoma Kusini hawafiki hata asilimia 10 ya wapiga
kura wote). Haya ndio madhara ya Katiba ya sasa. Katakana na historia
ya kisiasa baadhi ya watu wanajaribu kunihusisha na matatizo ya chama
cha NCCR-M. Napenda kuweka wazi kwamba sihusiki kwa namna yeyote ile na
migogoro ya chama kile.
Ninaomba
nisihusishwe na mambo yasiyonihusu. Ni dhahiri kwamba kuvuliwa
uanachama kwa David ni jaribio kubwa kwa mfumo wetu wa demokrasia kama
ilivyokuwa huko nyuma wakati kina Erasto Tumbo walipovuliwa uanachama
wa chama chao cha UDP. Ninaamini NCCR-M watamaliza matatizo yao kwa
mujibu wa katiba ya chama chao na ndugu David Kafulila atazikabili
changamoto hizi kama kiongozi kijana wa kisiasa na kuona hii kama fursa
badala ya kukata tamaa. Ifahamike wazi kabisa kwamba David ni mtu huru
mwenye mawazo yake na maamuzi yake. Kwamba sisi ni marafiki wa karibu
na kwamba tunatoka mkoa mmoja haina maana kwamba lolote afanyalo ama
nimemtuma au ninahusika.
Ninaheshimu misimamo yake na siku zote huwa nipo upande wa anayeonewa,
kudhulumiwa na mnyonge. Msimamo huu wa msingi usiwape watu nafasi ya
kunihusisha na mambo ya chama dhaifu kisicho na dira kama NCCR-M.
Kafulila akumbuke kwamba hakufukuzwa CHADEMA, alijiondoa mwenyewe.
Milango yetu ipo wazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za chama
chetu.
Ndg. Kabwe Zuberi Zitto, Mb
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)