Maonyesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yaendelea viwanja vya sabasaba - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Maonyesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yaendelea viwanja vya sabasaba

Mbunge Mstaafu wa Sumbawanga Mjini na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa na pia Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Waziri Paul Kimiti (kulia) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Anaa Mbelwa (kushoto) kuhusu mafanikio ambayo Wizara ya fedha imeyapata katika kipindi miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Afisa Mkuu Mfawidhi wa Benki Kuu Harry Mwansembo(kushoto) akimwonyesha Mbunge Mstaafu wa Sumbawanga Mjini na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa na pia Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Waziri Paul Kimiti (kulia) baadhi ya picha za noti zilizotumika tangu mwaka 1961 hadi leo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mbunge Mstaafu wa Sumbawanga Mjini na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa na pia Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Waziri Paul Kimiti (kushoto) akitazama baadhi ya picha za noti zilizotumika tangu mwaka 1961 hadi leo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kulia ni Afisa Mkuu Mfawidhi wa Benki Kuu Harry Mwansembo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages