Mkali
wa muziki wa hip hop kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini,
Mflame wa Rhymes, Simba Mzee, Afande Sele akiwarusha vilivyo wakazi
mbalimbali wa jiji la Mbeya, waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa
huduma mpya ya Airtel, Airtel Money uliofanyika jana jioni kwenye uwanja
wa mpira wa miguu wa Sokoine.
Kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Temeke, Wanaume Halisi
likiongozwa na kinara wao Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo jan
jioni ndani ya uwanja wa Sokoine, kwenye uzinduzi wa huduma mpya
itolewayo na kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel, ijulikanayo kwa jina
la Airtel Money, ambapo wakazi wa jiji la Mbeya wameipokea kwa shangwe.
Ilikuwa shangwe mwanzo mwisho, wakazi wa Mbeya wameipokea vyema huduma ya Airtel Money.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Jaffarai akitumbuiza jukwaani jana jioni
kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya kutoka kampuni ya simu ya
Airtel, ijulikanayo kwa jina la Airtel Money.
Wakazi
wa jiji la Mbeya kutoka vitongoji mbalimbali wakishangilia vilivyo jana
jioni kwenye tamasha hilo la Airtel Money, lililofanyika katika uwanja
wa Sokoine, jijini Mbeya.
Jukwaani
ni wakali wa miondoko ya hip hop katika muziki wa kizazi kipya, kulia
ni Jaffarai pamoja na Jay Mo wakikamua vilivyo jukwaani kwenye tamasha
la Bongo 50, lililodhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,
kupitia huduma yao mpya ya Airtel Money.
Palikuwa hapatoshi kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Picha Zote na Ahmad Issa Michuzi MICHUZI JUNIOR 




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)