Rais
aliyeondolewa madarakani nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo anafikishwa
mbele ya mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC hii leo. Mwansiasa huyo
anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita. Gbagbo
alipelekewa nchini Uholanzi wiki jana.
Mahakama
ya ICC imemtuhumu Gbagbo kwa makosa ya uhalifu wa kivita kufuatia
machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa Ivory Coast mwaka jana
alipopinga kuyakabidhi madaraka kwa mpinzani wake,Alassane Ouattara,
ambaye sasa ndiye rais wa Ivory Coast.
Kiongozi
huyo ambaye ndiye rais wa kwanza kufikishwa mbele ya ICC atasomewa
makosa yake chini ya sheria za mkataka wa Roma uliounda mahakama hiyo.
Baada ya kusomewa mashtaka yake itakuwa jukumu la majaji waandamizi
kuamua siku ya kusikizwa kwa kesi dhidi ya Laurent Gbagbo.
Nchini Ivory Coast wafuasi wa Gbagbo wametaja hatua ya kumkamata mwanasiasa huyo kama utekaji nyara wa kisiasa na kuonya hatua ya kumfungulia mashataka inahujumu mpango wa maridhiano ya kitaifa. Hata hivyo Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ya ICC anayeondoka Luis Moreno Ocampo amekanusha kauli hiyo na kusema kuna ushahidi tosha kumfungulia kiongozi huyo mashkata ya uhalifu wa kivita na siyo shinikizo za kisiasa.
Mahakama
ya kimataifa ya jinai ilianzishwa mwaka wa 2002. Hii ndiyo kesi ya
kwanza kubwa kusikilizwa katika mahakama hiyo.Baadhi wadadisi wameona
kama ushindi kwa mahakama hiyo huku baadhi nao wakiendelea
kulalalamikia utaratibu wa pole hususan katika utekelezwaji wa kesi.
Kuna wengine ambao wamelalamikia mahakama ya ICC kwa kuwalenga viongozi
na wanasiasa wa bara Afrika Pekee na kufungia macho mataifa mengine
hasa ya magharibi
BBC Swahili






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)