Kijana
Edwin Dossantos na mkewe waliojaliwa kupata watoto watatu mapacha mwezi
wa 7 mwaka huu ametoa shukrani zake za dhati kwa wasamaria wema wote
waliomsaidia kwa hali na mali kutoa michango kwa ajili ya malezi ya
watoto hao kutokana na halisi ya kipato chake kuwa cha chini na maisha
kuzidi kuwa magumu.
Akizungumza
na Sufianimafoto Reporter, ilipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kimara
jijini Dar es Salaam, Dossantos amesema ni msaada wa wasamaria wema
ndio umemuwezesha kumudu gharama za matumizi kwa ajili ya watoto hao
haswa ukizingatia hakuwa na kazi.
Aidha
Dossantos licha ya kuwashukuru wanao onekana katika orodha hii, pia
amewashukuru na wale ambao hawakutaka kujulikana waliomsaidia kupitia
mawakala wa M-Pesa pasipo kujitaja majina yao, ambao licha ya
kuwashukuru amesema hawakumtendea haki kwa kuwa wamemnyima fursa ya
kuwashukuru kwa majina yao wala namba zao.
Dossantos ametoa shukrani kwa watu waliosaidia kwa namna mbalimbali kama wanavyoonekana katika orodha ifuatayo.:-
Mr.
Frank wa DSM, Mrs. Norah wa Silver Boutique, Mama Sige wa KIBAMBA,
Mrs.Pamela wa USA, Mr. Sagday wa DSM, Mrs. Caroline Kazinza wa AZANIA
BANK-Tegeta, Mrs. Emakulata wa UK, Miss Nyota Omary wa NORWAY, Mr.
Joshua wa DSM, Mrs.Pamela wa DSM, Mrs.Mosha wa ARUSHA, Mrs. Lestituta wa
DSM, Mrs. Theresia na Mrs Zahara wa Hisense DSM, Mr. Shabiby wa GAIRO
Morogoro, Mrs. Fane wa DSM, Mrs. Ikupa wa AZANIA BANK-Tegeta DSM, Mrs.
Vale wa AZANIA BANK-Tegeta DSM, Miss Hoyce Temu wa Channel Ten DSM, Mrs.
Mercy Mariale wa DSM, Mr. Rongen Kambugu wa Kigali RWANDA, Advocate
Komba wa NSSF-DSM, Miss Jehn wa DSM, Mr. Freya Mahinya wa Zanzibar, Mr.
Chube wa DSM,Mr. Yusuph Mdoe wa DSM, Mr.Emmanuel Messo wa WORLD
BANK-DSM, Mr. Deogratius Rweyunga wa ITV-DSM, Mr. Iddi Kibwana wa
TTCL-DSM, Mr. Hashim Lundenga wa DSM na Bi. Asia Waziri Moyo wa
Zanzibar.
Hata
hivyo amesema watoto hao ambao kwa sasa wanaumri wa miezi 5 bado
wanahitaji msaada angalau hadi wafikishe umri wa miezi 6 ambapo watakuwa
wanaanza kula vyakula vya kawaida.
Katika
hatua nyingine Edwin Dossantos ametoa ombi kwa msamaria mwema
atakayekuwa na uwezo wa kumpatia nafasi ya kazi yoyote itakayompatia
kipato cha kuweza kumudu gharama za malezi ya watoto hao.
Amesema
bila ya yeye kuwa na kazi ya kumuingizia kipato anaweza kuja kwa
wasamaria kuomba misaada kila mara, hivyo ameshukuru kwa kumpatia kile
alichokiita samaki na sasa anaomba nyavu (Kazi) ili avue mwenyewe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)