John Ngahyoma(pichani), Mwandishi mkongwe wa habari Tanzania na Mtangazaji amefariki dunia hii leo asubuhi.
Kifo
cha Ngahyoma aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa shirika la Utangazaji
la Uingereza (BBC) nchini Tanzania akiripoti kutoka Dar es Salaam na
viunga vyake kimekuja siku moja baada ya mtangazaji mwingine mkongwe wa
kike aliyejizolea sifa kubwa ya utangazaji mpira Haklima Mchuka kufariii
ghafla huku mipango ya maziko yake ikiendelea.
Ngahyoma
aliyewahi kufanya kazi katika vituo vya taifa vya redio cha Redio
Tanzania Dar es Salaam na baade kujiunga na IPP Media katika vituo vya
Redio One na ITV ambako pia aliondoka na kujiunga na BBC ameripotiwa
kufariki hii leo jijini Dar es Salaam.
Tasnia
ya habari nchini Tanzania kwa kipindi cha siku mbili itakuwa imeapatwa
na pigo kubwa kufuatia vifo vya waanahabari hao wawili wa siku nyingi.
Marehenu
Ngahyoma amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu na hata kwenda nchini
India kwa matibabu zaidi kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsibu.
Taarifa
ya haraka iliyotumwa katika mitandao ya kijamii (blogs) na Katibu Mkuu
wa Jukwaa la wahariri (TEF) Neville Meena inasema msiba upo nyumbani kwa
marehemu Tabata Segerea jijini Dar es Salaam jirani na kwa Mwandishi
mwingine aliyefariki miezi kadhaa iliyopita Danny Mwakiteleko.
Aidha Meena ameomba mtu yeyote atakaekuwa na taarifa zaidi kuhusiana na mipango ya maazishi ya Marehemu Ngahyoma kumfikishia.
Blog
hii inaungana na wanahabari wote Tanzania na duniani kutoa pole kwa
familia ya marehemu akiwepo, mke, watoto, ndugu jamaa na marafiki wote
kwa msiba huo mkubwa uliowafika wakati huu wa shamra shamra za mwaka
mpya.
Mungu awatie nguvu na imani wote waliofikwa na Msiba huu.
Bwana Mungu alitoa na Bwana Mungu ametwaa Jina lake lihimidiwe.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)