Mdau
wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mjumbe wa Shirikisho la Muziki,
Francis Kaswahili akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Utafiti kwenye
Sekta ya Sanaa.
Na Aristide Kwizela
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limeeleza kuwa, kuna kila sababu ya Wasanii
kufanya utafiti wa kina kabla ya kuandaa kazi zao ili zikubalike kwa
walaji na si kujifurahisha wao wenyewe.
Mkurugenzi
wa Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA, Godfrey Lebejo (Katikati)
akizungumza na Wadau wa Jukwaa la Sanaa wiki hii kuhusu umuhimu wa
Utafiti kwenye sekta ya Sanaa. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Sanaa,
Aristide Kwizela na Kaluona Desdery
Wito
huo umetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na
Habari BASATA, Godfrey Lebejo wakati akizungumza na Wadau wa Sanaa
katika ukumbi wa BASATA uliopo Ilala Bungoni kwenye program ya Jukwaa la
Sanaa.
Lebejo alisema kuwa, utafiti ni
muhimu pale msanii anapotafuta wazo la kuandaa kazi ili kujua
itakubalika kiasi gani kwa jamii na ni ujumbe wa namna gani unakusudiwa.
“Msanii lazima afanye utafiti ili
ajue mlaji wa kazi yake anataka nini. Hauwezi kutengeneza kazi ili
kujifurahisha mwenyewe mwisho wa siku mlaji ni jamii inayokuzunguka”
alisema Lebejo.
Aliongeza kuwa, madhara ya wasanii
kutofanya utafiti husababisha kazi zao zisikubalike kwa jamii, zikose
masoko, zidumu kwa muda mfupi lakini pia kuipotosha jamii kwa ujumla
wake.
Aidha, aliongeza kuwa, vilio vya
wasanii juu ya ukosefu wa masoko ya kazi zao, kujirudiarudia kwa kazi
hizo na matatizo ya kunakili havitakwisha ikiwa wasanii hawatokuwa
tayari kutumia muda wao katika kufanya utafiti. Alisisitiza
kuwa, utafiti ni moja ya mbinu za kutafuta maarifa mapya na suluhisho
juu ya matatizo au changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususani
wasanii na sekta ya Sanaa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)