Kutoka
kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds FM/TV Shafii Dauda
alipokuwa akiwafanyia mahojiano mafupi kwa wachezaji wa mpira wa miguu
wa zamani ambao wameathirika na mafuriko yaliyotokea hivi
karibuni,anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Idd
Azan,Mwanamtwa Kihwelu (aliyewahi kuichezea timu ya Simba na
Yanga),Robert Damian (mwenye kofia-Simba),Mtangazaji wa kipindi cha
Michezo Clouds Fm/TV Ibrahim Masoud,Dua Said (Small Simba & Simba
S.C),Maalim Salehe a.k.a Romario (Yanga),Shaaban Ramadhan
(Simba,Yanga,Mlandege & Mtibwa) pamoja na Mke wa Marehemu Nico
Bambaga ambaye alikutwa akijishughulisha kutoa tope zito lililokuwa
limenasa kwenye nyumba yake aliyokuwa akiishi na familia yake.Wachezaji
wote hao akiwemo Peter Manyika ambaye hayupo pichani nyumba zao zote
zimeathiriwa vibaya na mafuriko.
Aliyewahi
kuwa mchezaji wa timu ya Yanga na Simba,Mwanamtwa Kihwelu akifafanua
namna adha ya mafuriko ilivyowakumba,mbele ya Mbunge wa jimbo la
Kinondoni,Mh Idd Azan,wakati kampuni ya Clouds Media Group ilipokwenda
kutoa misaada kwa waathirika na pia kujionea maeneo mbalimbali
yalivyoharibiwa na mafuriko hayo,mapema leo mchana jijini Dar,pichani
kati ni mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Bw.Ruge Mutahaba
ambaye pia aliongozana na baadhi ya wafanyakazi wa kampun hiyo mpaka
eneo hilo la tukio na kujionea hali halisi.
Mkurugenzi
wa Biashara Clouds Media Group,Dada Sheba akitoa salamu za pole kwa
Mbunge wa jimbo la Kinondoni,Mh Idd Azan kwa niaba ya baadhi ya Wananchi
wake walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar na
kusababisa madhahara makubwa,Aidha uongozi wa Clouds Media Group pia
ulikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mh Idd Azan pichani
kulia,mapema leo mchana kwenye kambi ya muda iliopo shule ya Msingi ya
Lutihinda,iliyowekwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.
Mmoja
wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa ameambatana
na baadhi ya wafanyakazi (hawapo pichani),akitoa maneno ya pole kwa
waathirika wa mafuriko pamoja na kuwaeleza misaada mbalimbali
walioitoa,aidha Ruge amesema kuwa pamoja na kutoa msaada huo wa
vyakula,nguo na mambo mengine,wataweka hema ambalo litahusika kwa ajili
ya kutolea huduma ya kwanza na pia kuwahamasisha wanajamii mbalimbali
watakaoguswa kujitolea kuleta madawa mbalimbali kwa ajili ya huduma ya
kwanza,kwani eneo hilo lina mkusanyiko mkubwa wa watu,hivyo mambo ya
magonjwa mbalimbali ikiwemo ya mlipuko yanaweza kutokea.
Mbunge
wa jimbo la Kinondoni,Idd Azan akizungumza na baadhi ya wananchi
waliothirika na mafuriko kwenye kambi yao ya muda iliyopo shule ya
msingi ya Lutihinda,Kigogo jijini Dar,ambapo kampuni ya Clouds Media
Group ilifika eneo hilo na kutoa msaada wa vitu mbalimbali,ambavyo
vilipokelewa na Mbunge huyo,Idd Azan
Pichani
juu na chini ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Dogo Ditto pamoja na
AT wakiwaimbia baadhi ya watoto walioko kwenye kambi ya muda ya
waliothirika na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar,kambi hiyo
imewekwa kwenye shule ya msingi Lutihinda,kata ya Kigogo wilaya ya
Kinondoni,ambapo kampuni ya Clouds Media Group ilikwenda kutoa msaa wa
vitu mbalimbali ikiwemo maji,vyakula,magodoro pamoja na nguo,aidha kama
vile haitoshi Clouds imeahidi kutoa msaada wa madawa mbalimbali na
kuweka hema la huduma ya kwanza katika kambi hiyo,ambapo waathirika
wamekusanyika eneo hilo kwa wingi lakini hakuna huduma yoyote ya kiafya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)