
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Lawrence Mafuru
--
Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
IMEELEZWA
kuwa Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa huduma za kibenki na
kukabiliwana changamoto kadhaa licha ya kuwepo mafanikio katika miaka 50
ya uhuru.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Lawrence
Mafuru alisema kuwa wakati wa uhuru Tanganyika ilikuwa na benki moja tu
ambayo ni Benki ya Taifa ya Biashara lakini baadaye kulijitokeza benki
kadhaa ambazo zilichangia kwa kiwango kikubwa kukuza maendeleo ya taifa
hili.
Alisema
NBC kwa kiwango kikubwa ilichangia kukuza maendeleo ya taifa hili kwani
ilishiriki kwa kiwango kikubwa katiuka ujenzi wa barabara na viwanda
jambo ambalo lilichangia kwa kiwango kikubwa sana ukuaji wa maendeleo ya
Tanzania.
Mafuru
alisema kuwa nchi inaadhimisha miaka ya 50 ya uhuru lakini benki ya NBC
itakuwa ikiadhimisha miaka 45 ya uwepo wake mapema mwakani jambo ambalo
inaonesha ukomavu na ukongwe wa benki hii.
“Kuna
mafanikio mengi sana ya kifedha ambayo tunajivunia licha ya nchi yetu
kuendelea kutajwa katika kundi la nchi masikini kwa takwimu za kimataifa
lakini ukweli ni kwamba tumeweza kusonga mbele kwa kiwango kikubwa sana
katika masuala ya kifedha ukilinganisha nia miaka 50 iliyopita”
alisema.
Alisema
kuwa NBC imeweza kupiga hatua kubwa kwani mpaka hivi sasa ina matawi 53
nchini yaliyounganishwa katika mtandao wa teknolojia ya kisasa ya
kibenki na kutoa huduma za kisasa zinazokidhi mahitaji kwa wateja
yanayoendana na wakati.
NBC
imeweza kutoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi zaidi ya 1500 jambo
ambalo limechangia ongezeko la kipato kwa watanzania na kupunguza tatizo
la ajira nchini.
Pia
Mafuru alisema kuwa NBC imekuwa mdau mkubwa wa huduma za kijamii hasa
katika huduma za Afya, Elimu na uwekezaji katika makundi ya wasio na
uwezo wa kumudu kupata huduma hizo muhimu nchini huku sulala la elimu
peke yake NBC ikitumia kiasi cha shs Bilioni tatu katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita.
Halikadhalika
Mafuru alisema kuwa NBC bado inaendelea kuwa mdau mkubwa katika
maendeleo ya taifa kwani kwa sasa inachangia upatikanaji wa makazi bora
kwa watanzania kwani hivi karibuni imeingia mkataba na Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) ili kuweza kujenga makazi bora na ya bei rahisi kwa
ajili ya watanzania.
Akizungumzia
changamoto zilizopo nchini Mafuru alisema Tanzania bado inahitaji
huduma za kibenki kwa kiwango kikubwa licha ya fikra ya kuwepo kwa
changamoto baada ya kampuni za simu kujihusisha na utoaji wa huduma za
kifedha, jambo ambalo alisema bado mahitaji ni makubwa sana. “Kwa sasa
tuna benki 45 tu nchini ambazo zinatoa huduma kwa asilimia 10 tu ya
watanzania hali hii inaonesha bado kuna mahitaji makubwa sana ya benki
nchini hapa” alisema Mafuru.
Pia
alisema hapa nchini kumekuwa na tatizo la kutokuwa na utamaduni wa
uwajibikaji licha ya kuwepo wasomi wengi lakini bado taifa linahitaji
watu wa kujitoa na kujituma zaidi katika utendaji wa kazi na kukuza
weledi ili kuendana na wakati huu wa utandawazi, jambo ambalo limekuwa
likitia hofu wengi kuwa nchi itakapoingia katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki watanzania wengi wanaweza kupoteza ajira hoja si kutokuwepo
kwa wasomi ila suala lipo katika uwajibikaji.
Alisema ikiwa watanzania watajituma na kufanya kazi kwa bidii hakuna haja ya kuogopa kwani watakuwa na uwezo wa kushindana.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)