Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi
Ombeni Yohana Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Balozi Sefue anachukua nafasi inayoachwa wazi na Bwana Phillemon Luhanjo
ambaye anahitimisha mkataba wake wa utumishi wa umma kesho, Jumamosi,
Desemba 31, 2011.
Kabla ya uteuzi wake, Balozi Sefue alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Kabla ya hapo, Balozi
Sefue alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na kabla ya hapo
alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tokea Oktoba 2005.
Balozi Sefue ataapishwa leo, Jumamosi, Desemba 31, 2011 saa nne asubuhi,
Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)