MWANAMUZIKI
wa kizazi kipya na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi a.k.a
Sugu anatarajiwa kuwapawisha mashabiki wa muziki huo jijini Arusha.
Sugu
akiwa na wasanii wengine wanatarajiwa kukonga nyoyo za mashabiki katika
viwanja vya Tripple A mjini hapa kwa kiingilio cha Sh. 5,000. Akizungumza
na vyombo vya habari jana mjini hapa Sugu aliwaomba wakazi wa Jiji la
Arusha kujitokeza na kuwaunga mkono wanamuziki walioamua kufanya
harakati za kupambana na kuukomboa muziki wa kizazi kipya.
“Tamasha
hili la “Anti Virus Burudani kwa mashabiki” linalenga kupiga kelele au
kufikisha ujumbe kwa Taifa ili watoke nje na kuungana na wasanii katika
kutetea kazi zao. “Kwa
miaka mingi wasanii wamekuwa wakilalamika kwenye nyimbo. Lakini sasa
tumerudi jukwaani kuonyesha bado wasanii hawajaishiwa kama inavyodaiwa,”
alisema Sugu.
Akielezea
matamasha mengine yatakayofuatia alisema baada ya kuzindua Dar es
Salaam Novemba 18 Mwaka huu, Anti Virus itapelekwa Jiji la Mbeya Desemba
24 Mwaka huu na baada ya hapo itakwenda Morogoro kisha Jiji la Mwanza. “
Nia yetu ni kuipeleka Anti Virusi nchi znima ili kuwatia moyo wasanii
wa maeneo ya mikoani mbali na Dar es Salaamu,” alisema Mr. Sugu.
Hata
hivyo Sugu alibainisha kuwa jambo moja analojivunia ni kuona wasanii
wakubwa na wenye majina katika muziki nchini wakimuunga mkono kwa kuamua
kujitoa muhanga kuibeba sanaa hiyo. “Asilimia
99. 9 ya wasanii wenye majina makubwa nchini wanatuunga mkono,
hatuwezi kuweka wazi mawasiliano hiyo ni siri unajua haya ni mapambano.
Baadhi
ya wasanii waliotajwa kuonyesha vimbwenga vya siku hiyo ni pamoja na
Suna G, Adili, Mkoloni, Mapacha, Dany Msimamo,Peen Lawyer, D wa Gheto,
Coin, Soggy Dogy, Rama Dee, Mr. Sugu mwenyewe na Isanga Family.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)