MTU mmoja amefariki katika moja ya ajali tatu zilizotokea leo katika
Barabara ya Mandela, jijini Dar es Salaam ambapo mwendesha pikipiki
alishindwa kuimiliki mashine yake hiyo na kuliingia gari kwa aina ya
Toyota Coasta kwa nyuma na kufa papo hapo.
Ajali nyingine ni magari ya jeshi la wananchi yamegongana baada ya gari la mbele kushika breki ghafla. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Ajali ya tatu ilikuwa kati ya daladala aina ya Toyota DCM lifanyalo safari zake kati ya Ubungo na Gongo la Mboto liligongana na teksi na kusababisha teksi hiyo kuharibika vibaya lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Daladala la DCM ambalo halikuharibika sana.
Wananchi wakiangalia gari lililo pata ajali.
HABARI/PICHA NA HARUN SANCHAWA, GPL

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)