Zanzibar Heroes kwenda Misri kwa maandalizi ya CECAFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Zanzibar Heroes kwenda Misri kwa maandalizi ya CECAFA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Future Century Ltd, Hellene Masanja (kushoto) akikabidhi jezi, viatu na vifaa vingine vya michezso kwa kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Stewart Hall (wa pili kulia) na Nahodha Msaidizi wa Heroes, Nadir Haroub ‘Canavaro’ (kulia) kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati (CECAFA). Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mjumbe Kamati Tendaji ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Abdalla Thabit Juma. Heroes inatarajiwa kuondoka jijini humo kesho kuelekea Misri kucheza mechi za majaribio za kimataifa kama sehemu ya maandalizi hayo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Future Century Ltd, Hellene Masanja (kushoto) na kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Stewart Hall wakiangalia moja ya jezi zilizokabidhiwa na kampuni hiyo kwa ajili ya maandalizi ya Zanzibar Heroes katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati (CECAFA). Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Wa pili Kulia ni Nahodha Msaidizi wa Heroes, Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Mjumbe Kamati Tendaji ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Abdalla Thabit Juma. Zanzibar Heroes inatarajiwa kuondoka jijini humo kesho kuelekea Misri kucheza mechi za majaribio za kimataifa kama sehemu ya maandalizi hayo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages