(Angalizo: Kwenye article hii nitatumia neno IT na ICT kumaanisha kitu kimoja)
Penda
usipende teknolojia imeleta mapinduzi makubwa sawasawa na wakati wa
industrial revolution. Nchi nyingi zimepiga hatua kubwa kwa kuona
umuhim wa kuwekeza kwenye sekta hii. Makampuni kama Amazon.com
yamechukua full advantage of IT kutengeneza mamilion ya hela, kutoa
huduma kwa jamii na kuajiri maelfu. Hata hivyo kusuasua na kusita
kuwekeza kwenye teknolojia kumedhoofisha nchi nyingi na makampuni mengi.
Japokuwa
hali ya uchumi wa dunia unayumba sana, watu wakiishi kwa hofu na
mashaka, ni muhimu kuendelea kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya
teknolojia. Viongozi katika sekta mbalimbali wamekuwa wakiona IT kama
kitu ambacho ni kizuri kuwa nacho lakini sio muhimu sana. Kwa sababu
hiyo imani imejengeka kwamba unawekeza zaidi kwenye IT pale unapokuwa
kwenye hali nzuri kiuchumi na kuacha ama kutokuipa ICT umuhimu pale
mambo ya kiuchumi yanapotetereka. ICT imekuwa victim kila inapotokea
bajeti imeyumba.
Kwa
kuendelea kuona kwamba IT au ICT sio chombo muhimu cha maendeleo, nchi
na jamii zetu zimekuwa zikishindwa kuendana na kasi ya teknolojia. Hata
tunapotaka sasa kuwekeza kwenye sekta hii wakati mambo yanapokuwa
mazuri kidogo tunakuwa tumeachwa nyuma sana.
Kuwekeza kwenye ICT kunahusisha mambo makuu mawili:
1. Research in technology - hii ina-stimulate innovation
2. ICT/IT consumption - hii inahusisha education; infrastructures; hardware and software acquisation; n.k
Tunawahimiza
viongozi kwenye private as well as public sector kubadilika na
kujifunza kutoka kwa wengine. Inawezekana bajeti haitoshi, lakini kwa
kui-sacrifice ICT ama kutokuona umuhimu wake ni vigumu ku-compete
kwenye hii dunia ya leo.
Tunapenda
kusisitiza kwamba ICT sio luxury bali chombo muhimu cha maendeleo.
Tuendelee kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya teknolojia
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)