Mapadri wakiwa wamebeba moja ya majeneza yenye miili ya
mapadri watatu na kijana mlei wakipeleka kwenye gari
kwenda kuhifadhiwa vizuri Hospitali ya Agakhan, baada ya
kuiombea katika ibada maalumu iliyofanyika jana Kanisa
la Katoliki Msimbazi, Dar es Salaam, tayari kusafirishwa nchini kwao
Italia kwa mazishi.Walikufa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria
kutoka Kongwa kwenda Dar es Salaam, iliyotokea hivi
karibuni eneo la Ruvu, Pwani, baada ya kugongana uso kwa uso na lori.
Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la
Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Salutaris Libena akiiombea miili ya
mapadri watatu na kijana mlei katika ibada maalumu
iliyofanyika jana Kanisa la Katoliki Msimbazi, Dar es
Salaam, tayari kusafirishwa nchini kwao Italia kwa mazishi. Walikufa
katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kongwa
kwenda Dar es Salaam, iliyotokea hivi karibuni eneo la Ruvu, Pwani,
baada ya kugongana uso kwa uso na lori.
Baadhi ya waumini wakilia wakati majeneza yenye miili ya
mapadri na Mlei mmoja ikipakiwa kwenye magari baada ya
kuombewa.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)