Bodi
Utalii Tanzania (TTB) ikishirikiana na kampuni mbalimbali za Utalii
imeshiriki maonesho ya Utalii yaliofanyika nchini Uingereza yajulikanayo
kama World Travel Market kuanzia tarehe 7-10, 2011.
Jumla ya kampuni 62 kutoka Tanzania bara na visiwani walishirikia
maonesho haya na Waziri wa Maliasili ya Utalii Mheshimiwa Ezekiel Maige
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mheshimiwa Abdillah
Jihad Hassan viongozi wa wa serikali waliohudhuria maonesho haya.
Katika maonesho haya Banda la Tanzania lilikuwa kati ya mabada makubwa
kwa upande wa Afrika na lilikuwa na picha zinazoonesha vivutio vya
Utalii vya Tanzania vilevile kulikuwepo bango kubwa linalohasisha Miaka
50 ya Uhuru wa Tanzania.
Banda la Tanzania lilivyooneka wakati wa maonesho yaliofanyika nchini
Uingereza tarehe 7-10 Nov 2011.
Banda
la Tanzania lilitembelewa na watu mashuhuri, mmoja wa watu mashuhuri
waliotembele banda la TTB ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ghana na Timu
na anayechezea soka lake katika timu ya Al Ain ya Falme za kiarabu (UAE)
i Asamoah Gyan. Asamoh akiwa na baadhi ya raia kutoka Rwanda na pamoja
na mmoja wa maafisa wa Bodi ya Utalii Mr Geofrey Meena kwenye maonesho
haya yaliofanyika Uingreza
Mmoja
wa washiriki waliohudhuria maonesho haya alikuwa Mkurungezi Mkuu wa
Cordial Tours and Travel Mr David Kizito hapa Mzee Kizito alikuwa
katika harakati za kuuza Safari za kuja Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)