TAIFA STARS WAREJEA DAR KUJIANDAA KUWAKABILI CHAD KESHOKUTWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAIFA STARS WAREJEA DAR KUJIANDAA KUWAKABILI CHAD KESHOKUTWA

Wachezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni baada ya kumaliza kazi ya kuaadhibu Chad nyumbani kwao kwa mabao 2-1. Stars imewasili leo na inaingia kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano na Chad unaotarajiwa kupigwa Jumanne Novemba 15 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Stars itahitaji sare ya ama ushindi wa aina yeyote ili kuweza kujihakikishia tiketi ya michuano hiyo.
Henry Joseph na Nizar Khalfan, wakitoka nje ya uwanja huo leo.
Kocha Mkuu wa Stars, Jan Poulsen, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius Nyerere.
Mashabiki wa soka wakiwa wamelizunguka basi la Stars mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages