Naibu
wa Waziri wa Mawasiliano Charles Kitwanga akizungumza na kocha wa shule
ya mpira wa klabu ya Manchester United Billy Miller alipotembelea
katika mafunzo ya kimataifa ya airtel rising stars kwenye Uwanja wa
taifa jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano Charles Kitwanga akisaliamiana na wachezaji wa
walioko katika mafunzo ya kimataifa soka inayoendeshwa na makocha wa
kutoka shule ya soka ya klabu ya Manchester United.
Kocha
wa vijana wa viungo kutoka shule ya soka ya klabu ya Manchester United
Paul Bright akiwatoka wachezaji wa wanaolioko katika mafunzo ya
kimataifa katika mazoezi ya jana
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Naomi
Njeri (kushoto) akimtoka Selemani Bufu jana wakati wa mafunzo ya soka
ya kimataifa yanayoendeshwa na makocha wa shule ya soka ya klabu ya
Manchester United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
SERIKALI imeIitaka Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kuhakikisha inawalea vijana waliopata nafasi ya kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya ‘ Airtel Rising Stars’ ili waweze kulisaidia taifa hapo baadaye.
Naibu Waziri wa Mawasiliano sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa, Charles Kitwanga alitoa kauli hiyo jana kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam alipokwenda kuwatembelea washiriki wa kliniki hiyo inayojumuisha mchi za Kenya, Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.
“Serikali inafurahi kuona mwekezaji kama kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na klabu ya Manchester United ya Uingereza zimejitokeza kusaidia maendeleo ya soka , hatuna budi kuhakikisha vipaji hivi vinaendelezwa pamoja na kukuza zaidi”, alisema Waziri Kitwanga.
Mheshmiwa Kitwanga alisema, jukumu la serikali ni kutoa miundombinu inayowezesha michezo kufanyika hivyo jukumu la kuhakikisha vipaji na elimu wanayoipata vijana hao inabaki kwa taasisi husika akimaanisha TFF.
“Serikali tunaahidi tutaendelea kutoa mazingira mazuri kwa hawa wawekezaji ili waweze kufanya kazi zao vizuri ili nao waweze kuhamasika na kuweza kusaidia kuwekeza kwenye sekta za michezo kama walivyofanya hawa wenzetu, “ alisema Mheshimiwa Naibu Waziri.
Alisema Tanzania na hata baadhi ya nchi nyingi za Afrika zimekuwa hazifanyi vizuri sana katika ngazi za kimataifa sio kwasabu hazina vijana wenye vipaji vya soka bali ni kwa sababu hazina program madhubuti za kuendeleza vijana ambao ndiyo mhimili wa maendeleo ya soka.

Mbali na Naibu waziri huyo, viongozi wengine walioitembelea kambi ya kliniki hiyo jana ni pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile, Osiah, Kocha wa timu ya soka ya Taifa nchini, ‘Taifa Stars’ , Jan Poulsen, Kocha mkuu wa timu za soka za Taifa za vijana nchini, Kim Poulsen, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Cheikh Sarr pamojana na viongozi wengine wa Airtel
Kliniki hiyo iliyozinduliwa na Oktoba 28 na mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, Bray Robson inatarajiwa kufungwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)