Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti
Breweriers (SBL) Richard Wells akizungumza na wahariri wa vyombo vya
habari na waandishi wa habari waandamizi wa michezo katika hafla ya
chakula cha mchana iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika hoteli ya JB
Bellmonte jijini Dar es salaam mchana wa leo.
Lengo la Mazungumzo hayo ilikuwa ni
kujadili mambo mbalimbali na kupata mchango wa mawazo kwa wanahabari
kabla ya kufanyika kwa mashindano ya TUSKER SECAFA CHALLENGE CUP
2011yatakayoanza hivi karibuni jijini Dar es salaam.
(PICHA ZOTE NA MOHAMED MAMBO)
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Ephraima Mafuru
akimkaribisha mkurugenzi wa kampuni hiyo ili kutoa maneno machache
katika hafla hiyo.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Tanzania TFF Angetile Osiah naye
alipata muda wa kuongea kidogo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akizungumza katika
hafla hiyo katika hoteli ya JB Bellmonte jijini Dar es salaam.
Wanahabari
wakijipakulia misosi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya
JB Bellmonte jijini Dar es salaam leo.
Umakini
ulikuwa muhimu hapa kama wanavyoonekana katika picha wakimsikiliza
Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto hayupo pichani , kutoka kulia ni Richard
Wells Mkurugenzi wa (SBL), Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL)
na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko (SBL).
Kutoka
kulia Juma Pinto Mwenyekiti wa TASWA, Richard Wells Mkurugenzi wa
(SBL), Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ephraim Mafuru
Mkurugenzi wa Masoko (SBL).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)