Rais Jakaya Kikwete
--
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Fabian
Massawe kufuatia vifo vya watu 18 kutokana na ajali ya barabarani
iliyotokea juzi, Jumamosi, Novemba 19, 2011, katika eneo la Lusahunga,
Biharamulo, Kagera.
Aidha,
Rais Kikwete ametuma salamu za pole kwa watu wote 17 walioumia katika
ajali hiyo ambako basi la Taqwa liligongana na lori kwenye barabara la
Biharamulo-Ngara.
Katika
salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mkuu huyo wa Mkoa, “ Nimepokea kwa
masikitiko na huzuni habari za vifo vya wenzetu 18 waliopoteza maisha
yao katika ajali ya basi la Taqwa. Kupitia kwako nawatumia salamu zangu
za pole za dhati ya moyo ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza watu
katika ajali hiyo,”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Wajulisheni kuwa niko nao katika uchungu mkubwa walionao
katika kipindi hiki cha maombolezo. Waambie kuwa msiba wao ni msiba
wangu pia. Nawaombeeni subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Namwomba Mwenyezi Mungu aziweka
roho za marehemu pahali pema peponi. Amen.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Kwa wenzetu walioumia katika ajali hiyo, nawatumia pole
zangu nyingi. Nawatakia heri waweze kupona haraka ili warejee katika
shughuli zao za kujenga taifa na za kujiletea maendeleo.”
IMETOLEWA NA:
NOVEMBA 21, 2011
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)