RADI YASABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI CHARLES MFAUME WA KITIVO CHA SAYANSI ZA JAMII CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA HAPO JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RADI YASABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI CHARLES MFAUME WA KITIVO CHA SAYANSI ZA JAMII CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA HAPO JANA

Picha Ya Marehemu Charles Mfaume 

Charles Mfaume ambaye alifariki hapo jana Mara baada ya kupigwa na Radi iliyoambatana na Mvua iliyonyesha Usiku wa jana Chuoni. Marehemu Charles Mfaume alikua ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa shahada ya kwanza ya biashara na utawala wa rasilimali watu. (BCOM HRM)

 Mwili wa Marehemu Unatarijiwa kuwasili Chuo Hapa Kwaajili ya Maombi na Kuagwa tayari kwa kusafirishwa kuelekea kwao Dar es Salaam tayari kwa mazishi. Sala na Zoezi zima la Kuaga mwili wa marehemu  kwa mara ya mwisho litafanyika muda si mrefu kwenye kiwanja cha mpira wa kikapu kilichopo katika kitivo cha sayansi ya jamii cha Chuo Kikuu Cha Dodoma leo na kusafirishwa leo

Vilevile Radi hiyo imesababisha wanafunzi wawili kulazwa zahanati ya chuo kutokana na majeraha aliyopata mmoja wa wanafunzi aliyefahamika kwa jina la Peter ambapo aliungua Mguu na Shingoni na Mwanafunzi mwingine Wa Kike huyu amelazwa baada ya kupoteza fahamu kutokana na mshtuko wa jana. Huu ni Msiba Wa Pili ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ndani ya Wiki moja Ambapo alhamisi iliyopita Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili Wa Kitivo Cha elimu Yohana Raphael kupoteza Maisha Ghafla mara baada ya kuanguka na kusafirishwa kwao Kigoma kwa Mazishi.

Timu nzima ya LUKAZA BLOG inapenda kutoa pole kwa uongozi wa chuo,familia, wanfunzi wenzetu pamoja na ndugu,jamaa na marafiki kwa kumpoteza mwanafunzi,ndugu yetu Charles Mfaume. Mungu atulinde na atutie nguvu katika kipindi hiki kigumu ambacho wanafunzi wa UDOM tunacho cha kupoteza ndugu zetu wawili ndani ya Wiki Moja.

Bwana alitoa na Bwana Alitwaa Jina la Bwana Lihudumiwe.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages