Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
inayoongoza ya usimamizi wa vyombo vya habari katika nchi za Afrika
Mashariki, Push Observer imemtangaza gwiji la sekta hiyo Duniani, Joe
Taylor kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wake.
Akizungumza jijini jana, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Push Observer, Omari Salisbury alisema kuwa hatua
ya kumwajiri Taylor imetokana na historia yake nzuri katika sekta hiyo
nchini Marekani na kampuni yao inataka mafanikio makubwa katika sekta
hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Salisbury
alisema kuwa Taylor ambaye kwa sasa amekwisha anza kazi, alikuja
nchini kwa mara ya kwanza mwezi Septemba na kuendesha ‘semina’ kwa
wadau mbali mbali kwenye hotel ya Sea Cliff na kuwafumbua macho wadau
wengi wa sekta hiyo.
Alisema
kuwa wanaamini kuwa ujio wake na kufanya kazi na kampuni hiyo
kutawawezesha kupata maendeleo makubwa huku wakitoa huduma bora zaidi
katika Nchi za Afrika Mashariki.
“Lengo
ni kupata maendeleo makubwa katika sekta ya usimamizi wa habari,
tumeamua kuajiri mtu bora kabisa kwa lengo la kutoa huduma bora kabisa,
naamini wadau wetu wakiwemo waandishi wa habari watapata kile
wanachokihitaji katika kazi zao,” alisema Salisbury.
Alisema
kuwa Taylor ni kiongozi bora na amekuwa katika fani hiyo kwa miaka 30
nchini Marekani. Kabla ya kujiunga na Push Observer, alikuwa mkurugenzi
wa kampuni ya VMS na mwaka 2009 walifanikiwa kushinda tuzo ya mwaka ya Innovation (Innovation of the Year Award) na mwaka huo huo wakashinda tuzo ya Cost Saving Award.
Talylor
vile vile amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ikiwa pamoja na makamu
wa Rais wa kampuni ya Broadcast Monitoring for Medalink na Rais wa Broadcast News Mid-America, Oklahoma.
Taylor
alisema kuwa amefurahi kujiunga na Push Observer na kufanya kazi
Tanzania na anaamini kuwa kampuni hiyo itafika mbali kwa kupata
maendeleo makubwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)