NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu (MB) akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO ya nyanda za juu kusini inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya. Kulia kwake anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana. Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini na wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi. 
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO nchini Ndugu Mike Laizer akifafanua jambo kwa Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye banda la SIDO. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana.

Uhifadhi wa Mazingira nao umepewa kipaumbele Mkoani Rukwa, Mjasiriamali wa uhifadhi wa Mazingira wa kikundi cha REYO akinadi miti aina mbalimbali inayofaa kwa uhifadhi wa mazingira na matumizi mengineyo katika maonesho hayo.
Maonyesho hayo yakiendelea

Mjasiriamali wa Rukwa anayejishughulisha na utengenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi mbalimbali. Chipawas Leather Tunning wanapatikana maeneo ya Jangwani Wilayani Sumbawanga, wapo pia kwenye maonesho hayo.

Haya mambo ya ajabu pia yapo, inadaiwa ni Mtu wa ajabu kutoka Burundi aliyezaliwa kichwa kitupu, ana uwezo wa kuzungumza lugha tofauti na wakati wa kumuhoji alidai kuwa chakula chake ni Sindano maalum. Katika akili ya kawaida haifikiriki na wengi wa watu waliomtembelea huyu bwana ikiwa ni pamoja na mimi walisema haya ni MAZINGAUBWE. Huyu bwana anapatikana kwenye banda moja na ili kuweza kumuona inatakiwa kulipia shillingi mia tano tu. Nilishuhudia baadhi ya watoto waliopata bahati ya kumuona wakilia kwa hofu na wengine wakiwa na mshangao mkubwa.

Naibu Waziri akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga. Kwa habari zaidi nenda hapa: (http://rukwareview.blogspot.com/)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages