MSIBA CHUO KIKUU CHA DODOMA NA KITIVO CHA ELIMU CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MSIBA CHUO KIKUU CHA DODOMA NA KITIVO CHA ELIMU CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA LEO

Wanafunzi wa Kitivo Cha Elimu Wakiwa katika Misa ya Kumuombea Marehemu Yohana Raphael ambaye alifariki dunia hapo jana katika zahanati ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mara baada ya Kudondoka ghafla wakati akitoka kula. Mara baada ya kudondoka aliweza kuwahishwa katika zahanati hiyo ya chuo iliyopo kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha lakini kwa bahati mbaya aliwezaa kupoteza uhai wakati kashafika katika zahanati hiyo.
  
Baadhi ya Wanafunzi wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakisubiri Kuupokea Mwili Wa Marehemu Raphael kwaajili ya misa na kuaga mwili huo tayari kwa safari ya kuelekea kwako kwa mazishi
Mwili wa Marehemu Yohana Raphael ambaye alikua ni mwanafunzi wa Mwaka wa 3 aliyekuwa akisomea shahada ya kwanza ya elimu ukiwa umewasili katika kitivo cha elimu tayari kwa wanafunzi na wafanyakazi kuaga mwili na misa ya kumuombea marehemu.

Timu nzima ya Lukaza Blogu ikishirikiana na Wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Inapenda kutoa pole kwa uongozi wa Chuo, Wanafunzi wote na Ndugu, jamaa na Marafiki katika kipindi hiki kigumu ambacho sisi kama wanafunzi tumehuzunishwa sana na msiba huu mzito.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina La Bwana Lihudumiwe



1 comment:

  1. Anonymous10:00 AM

    poleni sana Mungu awape wa uvumilivu na subira, kwani yeye humchua yule ampendae. Mungu ailaze rohoya marehemu mahala pema peponi AMEN.....

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages